ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 28, 2017

TANZIA: MWANDISHI WA HABARI CHANNEL TEN VALENCE ROBERT AFARIKI DUNIAAliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoa wa Geita,Vallence Robert Amefariki dunia Hii Leo Tarehe 28/03/2017, akiwa nyumbani kwao Muleba Kagera. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake Ribarikiwe..


Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Geita Daniel Limbe amethibitisha taarifa za kifo cha mwandishi wa habari Valence Robert.

Limbe ameiambia Maduka online  kuwa Valence Robert  hivi karibuni aliondoka mkoani Geita akiwa  anaumwa.


Hata hivyo inaelezwa kuwa Valence Robert alikuwa anaumwa ugonjwa usiojulikana.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwao Misenyi.

Hivi karibuni Valence Robert na Joel Maduka walipigwa na askari polisi wakati wakiwatawanya wananchi kwenye maeneo ya stendi ya zamani Mjini Geita ambao walikusanyika kusalimiana na Waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya  Chadema Edward Lowassa.
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.