ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 31, 2017

TATHIMINI YA JUMLA KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2016-2017

Dkt. Charlse Msonde, Katibu Mtendaji NECTA.

BARAZA
la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Dkt. Charlse Msonde, Katibu Mtendaji NECTA

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa watahiniwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya mtihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Aidha amesema baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa 126 waliobainika kufanya udanganyifu ikiwa ni pamoja na watahiniwa 58 wa shule, 58 wa kujitegemea na watahiniwa 10 wa QT. Pia baraza hilo limefuta matokeo ya mtahiniwa mmoja aliyebainika kuandika matusi kwenye karatasi yake ya majibu.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.

Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam

Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.