ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 16, 2016

WATOTO 60 WALIOPEWA MAFUNZO YA KIGAIDI, WANASWA.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro.
Jumla ya watoto 60 wamekamatwa katika kipindi cha mwaka mmoja na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakiwa wameachishwa masomo na kuingizwa katika mafunzo ya kigaidi ikiwemo kulenga shabaha kwa kutumia silaha na uporaji.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro amesema jeshi hilo limefanikiwa kuvunja kambi ya ugaidi inayowatumia watoto katika pori la Kilongoni Vikindu na kuwakamata wanawake 4 wakiwa na watoto 4 ambao wameingizwa katika mafunzo ya ugaidi.

Amesema watoto hao wamefundishwa kumaliza mtu pumzi na kufariki haraka, kutumia silaha ya SMG na bastola na kulenga shabaha.

Kamanda Sirro amesema mara baada ya kufanya mahojiano na watoto hao wamebaini wengine kutotambua walikotoka, huku jeshi hilo likiendelea kuwa tafuta watoto wengine ambao bado wanashikiliwa na magaidi katika kambi zingine.

Aidha, jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu 5 wakiwa na silaha pamoja na shilingi milioni 10, na pia limevunja mtandao wa wizi wa magari.

Hali kadhalika Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salama limefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi 587,520,000 kupitia tozo za makosa ya usalama barabarani kwa muda wa wiki moja kuanzia Desemba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.