ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 7, 2016

AJALI YAUA WATU 18, YAJERUHI WATATU.

By Stella Ibengwe na Suzy Butondo, 
CHANZO/Mwananchi 
Shinyanga.

WATU 18 wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Nsalala Mkoani Shinyanga.

 Ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Toyota Noah na lori la mizigo ilitokea juzi saa 1:30 usiku baada ya dereva wa Toyota Noah iliyokuwa ikitoka Nzega kwenda Tinde mkoani Tabora, Seif Mohamed (32), kujaribu kuyapita magari mengine na kugonga uso kwa uso na lori lililokuwa likiendeshwa na Aloyce Kavishe, mkazi wa jijini Dar es Salaam. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne alisema polisi inawashikilia madereva wote wawili kwa mahojiano na hatua za kisheria zitachukuliwa baada ya upelelezi kukamilika. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.