ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 21, 2016

VIJANA WAJASILIAMALI TOKA WILAYA YA MAGU WAVUNJA REKODI KWA MIRADI.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na huduma za jamii (NHC) Bi. Susan Omari akikabidhiwa Taarifa ya Mradi.
Nyumba zilizofanikiwa kujengwa.
Ufyatuaji matofali.
Taarifa...
Ukaguzi na eneo la mradi.
Moja ya nyumba zilizojengwa kwenye mradi.
Madi ukikamilika hatua kwa hatua.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na huduma za jamii (NHC) katika picha ya pamoja na wadu wa mradi.
TAREHE 20.10.2016

Zaidi ya vijana 40 wanaounda vikundi vitatu vya ujasiriamali wilayani Magu mkoani Mwanza, vilivyokabidhiwa Mashine moja ya kufyatulia matofali, chini ya mpango wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC), wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi.

Hii ni historia mpya iliyotengenezwa na vijana hawa ya kutotegemea ajira za Serikali kwa kujiajiri, baada ya kukamilisha ujenzi wa nyumba sita za gharama nafuu, zilizowawezesha kuwapa sifa ya kupata zabuni za ujenzi wa nyumba nyingine bora za kisasa nje na ndani ya nchi.

Akikamilisha ziara ya kukagua miradi hiyo, mkuu wa kitengo cha mawasiliano na huduma kwa jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa Susan Omari, amesema wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, na hivyo kuviongezea vikundi hivyo mashine mbili za kufyatulia matofali.

Vikundi hivyo vimewezeshwa, ili kuondokana na kilio cha ukosefu wa ajira, lakini pia kuwaepusha vijana na makundi yanayojihusisha vitendo vya uhalifu ikiwemo suala la matumizi ya dawa za kulevya, wizi na ujambazi.

Mkakati wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) ni kuhakikisha vijana katika maeneo mbalimbali nchini, wanaondokana na tatizo la kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa ajira kwa kujiajiri wao wenyewe katika shughuli mbalimba za ujasiriamali.

NA ZEPHANIA MANDIA
GSENGO BLOG.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.