ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 20, 2016

WANAFUNZI PAMBA SEC WARIPOTI VIPIGO.


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya pamba jijini mwanza wameiomba serikali kukomesha vitendo vya ukatili wanavyotendewa na walimu wao ikiwemo  vipigo kupita kiasi pamoja na baadhi yao kuvuliwa nguo wakati wa kuchapwa viboko.

Wakizungumza wakati wa mdahalo wa kujadili ukatili wa kijinsia, baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa ukatili wanaotendewa na walimu wao umekuwa ukichangia mahudhurio hafifu shuleni na hivyo kusababisha wengi wao kushuka kitaaluma.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya pamba iliyoko jijini mwanza wakijadili vitendo vya ukatili wanavyotendewa na jamii,wazazi pamoja na walimu wao.

Baadhi ya wanafunzi hao wametumia fursa hiyo kulalamikia ukatili wa vipigo kutoka kwa walimu wao.

Wakizungumzia malalamiko hayo,baadhi ya walimu wa  sekondari ya pamba wakawa na neno.

Mdahalo huo uliandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI ambapo mkurugenzi wa shirika hilo YASINI ALLY  amewashauri walimu wa shule hiyo kuimarisha mahusiano  yao na wanafunzi.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya pamba pia wameeleza kutendeana ukatili wao kwa wao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.