ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 20, 2016

MPAMBANO WA ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID.

MPAMBANO WA LEYLA RASHID NA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI HII …ni vita ya “Sura Surambi” na “Nina MoyoSioJiwe” 

NI vita ya “SuraSurambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”. Ndiyo unavyoweza kusema kuelekea mpambano wa waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi.

Onyesho hilo linasosubiriwa kwa hamu kubwa litafanyika Jumamosi ya  tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar esSaalam.

Bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic ndiyo zitakazosindikiza mpambano wa mahasimu hao wawili.

“SuraSurambi” ni moja ya nyimbo ambazo piga ua lazima iwe kweye ratiba ya Isha Mashauzi wakati iweisiwe Leyla naye lazima aidumbukize ngoma yake ya “Nina Moyo Sio Jiwe” katika orodha ya nyimbo atakazo tumbuiza.

Tangu onyesho hilo litangazwe, waimbaji hao wameingia kwenye vita vikubwa vyama neno ambapo kila mmoja amejinasibu kuibu kana ushindi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.