ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 4, 2016

HII NDIYO TATHMINI YA UHALIFU MKOA WA MWANZA.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.

Na Mwandishi wetu.
 MKOA wa Mwanza  kwa kipindi chaa mwezi Juni  mwaka huu umekuwa shwari ikilinganishwa na ya mwezi mei mwaka huu. katika matukio ya uhalifu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi  amesema kuwa pamoja na kuwa usalama kulikuwepo na baadhi ya matukio makubwa ya jinai kama mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha, unyang’anyi wa kutumia nguvu, uvunjaji,kubaka na wizi wa mifugo.

Amesema licha ya kuwepo kwa hata hivyo matukio  ya uhalifu yaliweza kushughulikiwa na jeshi la polisi wakishirikiana na wadau wa ulinzi na usalama vizuri, kwani baadhi ya watuhumiwa wa uhalifu walikamatwa na kufikishwa mahakamani, ambapo baadhi ya kesi zimemalizika na nyingine zinaendelea katika hatua tofauti mahakamani.

Taarifa hiyo ilisema kuwa watuhumiwa walioguswa na ushahidi na kukimbia baada ya kutenda matukio ya uhalifu wanaendelea kutafutwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na wananchi wenye nia njema ya kukabiliana na uhalifu katika mkoa wetu wa mwanza.

Katika matukio  katika kipindi cha mwezi juni, 2016 jumla ya makosa 3753 yaliripotiwa, wakati kwa mwezi mei, 2016 makosa 3798 yaliripotiwa, hivyo  kunaupungufu wa makosa 45, sawa na asilimia 1.2%.

Makosa yaliyotikisa makosa makubwa kwa kipindi cha mwezi juni, 2016 yalikuwa ni 232 ikilinganishwa na ya mwezi mei, 2016 ambapo makosa makubwa 197 yaliyoripotiwa, hivyo kunaongezeko la makosa 35 ambayo ni sawa na asilimia 15.8%, aidha katika kipindi cha mwezi juni,2016 makosa madogo yaliyoripotiwa ni 3521 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016.

Makosa ya Kawaida madogo 3601 yaliripotiwa, hivyo kunaupungufu wa makosa 80, sawa na asilimia 2.2%. hata hivyo upungufu huo unatokana na jitihada za jeshi la polisi kubuni na kutumia mbinu mpya za kupambana na uhalifu ambao umekua kutokanana kukua kwa teknologia pamoja na mbinu za kihalifu.

Makosa yanayotokana na jitihada za jeshi la polisi wakishirikiana nawadau wa ulinzi pamoja na wananchi kupitia misako na doria, makosayapatayo 108 yaliripotiwa katika kipindi cha mwezi juni, 2016 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapo makosa 77 yaliripotiwa, hivyokufanya kuwa na ongezeko la makosa 31 sawa na asilimia 29%.

makosa makubwa na madogo ya usalama barabaranikwa upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa yote yaliyoripotiwa mkoani mwanza katika kipindi cha mwezi juni, 2016 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji ni 11,100 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapoyaliripotiwa jumla ya makosa 10,490, hivyo kunaongezeko la makosa 1,390 sawa na asilimia 12.5% matukio ya ajali za barabarani yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwezi juni ni 12, ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 matukio yaliyoripotiwa yalikuwa 13 hivyo kunaupungufu wa tukio 01 sawa na asilimia 08%. matukio ya ajali za vifo yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwezi juni,2016 ni 10.

Amesema ikilinganishwa na mwezi mei 2016 ambapo pia yalikuwa 10.watu waliokufa kwenye ajali kwa kipindi cha mwezi juni, 2016 ni 15 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 walikuwa 11, hivyo kuna ongezeko la vifo vya watu  wane  sawa na asilimia 27%.

Katika kipindi hicho watu waliojeruhiwa kwa kipindi cha mwezi juni, 2016 ni 21 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapo walijeruhiwa watu 06 hivyo kunaongezeko la watu 15 sawa na asilimia 71.4% .

Katika  kipindi cha mwezi juni, 2016 jumla ya makosa 11,088 yalikamatwa na kutozwa faini na kiasi cha tsh.329, 790,000 ikilinganishwa na mwezi mei 2016 ambapo jumla ya makosa 10,389 ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo ya shs. 311,670,000, hivyo kunaongezeko la makosa 699 na ongezeko la maduhuri ya sh. 20,970,000 sawa na asilimia 6.3% jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani baadhi yao wanaendelea kuficha wahalifu na uahlifu katika maeneo yao na kutokuwa tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa asilimia 100.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.