ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 12, 2016

FAHAMU HAYA MACHACHE KUHUSU MTOTO WA OSAMA ALIYEAPA KULIPA KISASI.

usamaJina kamili:-
Hamza bin Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden, kwa kifupi Hamza Bin Laden mtoto wa Osama bin Laden, alizaliwa mwaka 1991 na moja kati ya wake watu wa Osama, Khairiah Sabar wa Saudi Arabia ambaye alikamatwa na kuenda kuhojiwa walivyokuwa wakiishi Abbottabad ambako walivamiwa na majeshimnamo tarehe 2 mwezi Mei 2011 wakati akiwa na miaka 20, na ikagundulika ni Hamza pekee ndio hakuwepo mahali pale kwa wakati huo.
Mahusiano yake na Al Qaeda:-
Mwaka 2005 alionekana kwenye video iliyopewa jina la The Mujahideen of Waziristan, ambako Hamza alionekana akishirikiana na Al-Qaeda kuwashambulia walinzi wa Pakistan huko Kusini mwa Waziristan. Na ilipofika 2007 alipewa nafasi katika uongozi wa kundi la Al-Qaeda walipokuwa kwenye mipaka ya Afghanistan/Pakistani alihusishwa na mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakstani Benazir Bhutto, na kwa mujibu wa msemaji wa Al Qaeda Sulaiman Abu Ghaith, Hamza alikua ameshikiliwa huko Iran wakati Bhutto anauawa na hakuachiwa mpaka 2010.
Gazeti la The Sun lilichapisha shairi linalosemekana kuandikwa na Hamza ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 25, liliwekwa kwenye tovuti ya Waislamu wenye msimamo mkali. Na ndani ya shairi hilo Hamza aliandika ‘Accelerate the destruction of America, Britain, France and Denmark’ akimaanisha kwamba atashiriki kwa kasi uharibifu wa nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa na Denmark na kwa kumjibu Patrick Mercer ambaye ni mbunge nchini Uingereza aliamua kumpatia jina la ‘The Crown Prince of Terror’ yaani aliamua kumvika taji la Ukuu wa ugaidi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.