ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 8, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: IDD AZIZ AACHIA VIDEO MPYA “KISWAHILI”


Unafahamu Kiswahili? Mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Idd Aziz kutoka nchini Kenya ameachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Kiswahili.’ Ukihusu lugha adhimu ya Kiswahili, wimbo huu maridhawa umedhamiriwa kuwaunganisha wapenzi wa muziki na wajuzi wa lugha hiyo duniani kote.

Idd anauelezea KISWAHILI, “Nilitaka kutengeneza wimbo ambao hautaishia kuwa mzuri tu lakini pia uwe na ujumbe mkubwa utakaodumu kwa vizazi vingi.  Nahisi kuwa wanamuziki wa Kenya wakati mwingine huchukulia poa lugha za nyumbani, hasa Kiswahili hivyo huu utatukumbusha maana mahsusi ya Kiswahili na tafsiri yake ya pekee.”

Ukiandikiwa na kuimbwa na  Idd Aziz, KISWAHILI umetayarishwa na Jesse wa Revive Media huku video yake ikiongozwa na Sync. Kwenye video yake, Idd anaigiza kama mwalimu wa shule ya msingi huku hadithi yake ikitupeleka darasani ambako kupitia wimbo, anawafundisha wanafunzi umuhimu wa kushika urithi wetu kwa kujifunza Kiswahili.

Vitabu mashuhuri vya Kiswahili vya mtaala wa Kenya vinaonekana kwenye video hii iliyoongozwa kwa umahiri mkubwa.

KISWAHILI ni wimbo halisi wa Kikenya wenye vionjo vya Afrika Mashariki. “ Wimbo na ujumbe wa wimbo huu vimeshiba. Naamini mtaupenda. Nitaendelea kuachia nyimbo nzuri za Kiswahili,” anasema Iddi.

TAZAMA KISWAHILI kwenye YouTube: http://bit.ly/21DGSGB
BOFYA PLAY KUSIKILIZA 


Tafadhali pokea wimbo na art work yake vilivyoambatanishwa kwenye wimbo huu. Kuwa huru kuusambaza ndani ya mitandao yako.

USIKILIZE KISWAHILI kwenye Soundcloud: http://bit.ly/1O2zPok

DOKOZE KWA WAHARIRI:

Idd Aziz ni miongoni mwa wacheza ngoma maarufu Kenya akiwa mkuu wa bendi yake mwenyewe huku pia akiwa mcheza ngoma wa Sauti Sol. Kwa sasa anazunguka na kundi la Sauti Sol nchini Kenya kwenye ziara yao, Live and Die in Afrika.  Iddametumbuiza mara nyingi kwenye ziara za Afrika, Ulaya na Amerika. Amefanya kazi na wasanii nguli akiwemo Mercy Myra. Anasema anaendelea kujiimarisha pia kama mwanamuziki wa kujitegemea na kuingia studio kurekodi zaidi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.