ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 23, 2016

MOISE KATUMBI AHUKUMIWA MIAKA 3 JELA

Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi.
Pia alipigwa faini ya dola milioni 6.
Katumbi hakuwepo mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda Afrika Kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti wa kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.
Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kupanga njama dhidi ya serikali.
Katumbi amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.