ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 21, 2016

GEORGE SIMBA CHAWENE MGENI RASMI TUZO ZA UWEZESHWAJI KIUCHUMI NA AJIRA ZITAKAZO FANYIKA MWANZA.

Moja kati ya ahadi kuu za Serikali ya awamu ya 5 ya Rais John Pombe Magufuli ni 'Tanzania yenye Viwanda' 

Sera hii ukiitizama kwa juujuu unaweza dhani kuwa kama imewekwa kapuni hivi, lakini ukizama kwa ndani utagundua kuwa kuna mambo makubwa yanayoendelea kuhakikisha hilo linafanikiwa.

Bega kwa Bega Microfinance ni moja ya makampuni yanayoisaidia Serikali katika kuwezesha kutoa na mbinu za ujasiliamali kwa vijana.

- Kuwezesha ujenzi na upatikanaji wa mitaji ya uwekezaji na biashara kwa wananchi.
- Kuondoa ugumu wa upatikananaji wa mitaji ya hasa unaowakumba vijana na kadhalika.

Johakim Jonathan ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Bega kwa Bega hapa anafunguka zaidi ni jinsi gani anasimama kuhakikisha sera ya TANZANIA YA VIWANDA inafanikiwa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA


Mabone James ni Afisa Mtendaji Mkuu BKB Quality Capital.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simba Chawene anatua jijini Mwanza mwishoni mwa wiki ambapo mnamo Jumamosi hii ya tarehe 23 Juni 2016 anatarajiwa kukabidhi Tuzo za Uwezeshwaji Kiuchumi na Ajira zitakazo tolewa na Shirika la Bega kwa Bega Microfinance Ltd wakishirikiana na Convenant Bank.


Eneo la shughuli hiyo ni viwanja vya PPF Kiseke jijini Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.