ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 25, 2016

Na Albogast Benjamin Abo'g A plus B

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta amewaomba mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi siku ya jumatatu ili kuwapa nguvu kwa kuwashangilia na kuonyesha uzalendo ili waweze kushinda mchezo huo.

Samatta akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere punde tu baada ya kutua na kikosi kizima cha Taifa Stars wakitokea Chad majira ya saa 9 usiku alifanya mahojiano na jembe fm akisisitiza kuwa jumatatu wapo tayari kucheza na kushinda, "Tumejipanga kwaajili ya mchezo na mchezo ndio maisha yetu" alisema Samatta.

Naye kocha wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa alipata nafasi ya kuzungumza na Jembe fm na kubainisha kuwa kikosi chake kinakabiliwa na majeruhi wawili ambao ni Mwinyi Kazimoto na Kelvin Yondan lakini hali zao zinaendelea vizuri hivyo anasubiri ripoti ya daktari ili kujua kama watacheza siku ya jumatatu.

Mashabiki wengi walijitokeza kuanzia mishale ya saa 5 za usiku wakiwasubiri Stars kwa hamu na kikundi maarufu cha ushangiliaji cha Tanzania Football Suporters Association kilikuwepo kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawia ambapo mwenyekiti wao aliwaomba watanzania kujiunga na kikundi hicho ili kutoa hamasa kwa wachezaji kujituma zaidi.

Tanzania ina pointi 4 kwenye kundi G ikiwa imecheza mechi 3 huku ikiomba mchezo wa ijumaa kati ya Nigeria na Misri umalizike kwa sare kisha wao washinde mechi ya jumatatu dhidi ya Chad ili kujiweka pazuri zaidi kwenye hatua hii ya kufuzu Afcon 2017.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.