ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 15, 2014

PEPSI KOMBE LE MEYA 2014. SASA YAINGIA NGAZI YA NUSU FAINALI

Mashabiki wa Mnadani Fc wakiwa wamembebe mchezaji wao Alawi Mohamed ambaye aliwanyanyua mara mbili mashabiki hao toka vitini hatimaye ushindi katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Pepsi kombe la Meya 214 dhidi ya timu ya Magazeti, hadi mwisho wa mchezo Mnadani Fc 2, Magazeti 1.
Mpira wa adhabu ukipigwa kuelekea langoni mwa timu ya Magazeti Fc, katika mchezo wa robo fainali Pepsi kombe la Meya 2014, uliochezwa jana Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza,  Matokeo ya mchezo huo Mnadani Fc 2, Magazeti 1.
'Mpira uwekwe kati' kwa mujibu wa mwamuzi wa mchezo, mara baada ya goli la kwanza la kusawazishwa na Mnadani Fc ikiwa ni dakika saba tu toka Magazeti Fc  walipopata goli la kuongoza, baadaye Mnadani Fc waliongeza bao la pili na laushindi hivyo hadi mwisho wa mchezo Mnadani Fc wakasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa 2-1.
Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 imefikia patamu, sasa ni katika hatua ya nusu fainali.

Timu zilitinga nusu fainali ya michuano hiyo ni:-
1.Sokoni FC 
2.Mkolani
3.Mirongo pamoja na 
4.Mnadani Fc.

Michezo ya nusu fainali ya Pepsi Kombe la Meya 2014 itachezwa tarehe 16 na 17 mwezi huu ile hali fainali itakuwa jumamosi ya tarehe 20 katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Zaidi (BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA YA UWANJANI)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.