ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 22, 2014

UONGOZI WA JIJI LA MWANZA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHA WAMALIZA MGOMO.

Sehemu ya mbele toka lango la kuingilia Ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza.
*Jiji lapiga marufuku matoroli na mikokoteni.
*Huduma ya Vyoo sasa Sh 200
*Uchangiaji uzoaji taka Sh 8,000 kwa mwezi kila duka   mjini kati.
NA PETER FABIAN, MWANZA.
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza limekataa kuondoa sheria zake zilizopo ili kutekeleza baadhi ya matakwa ya hoja zilizowasilisha na Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) zilizopelekea mgomo wa kufungwa maduka kwa siku mbili jiji hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hassan Hida, kutoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilishwa kwenye kikao cha pamoja na viongozi wa Jumuiya hiyo kufatia mgomo wa siku mbili uliopelekea maduka jijini hapa kufungwa.

Hida alisema kwamba katika kikao hicho na wawakilishi wa wafanyabiashara wa jumuiya,  hoja mbalimbali za wafanyabiashara zilizowasilishwa na mwanasheria wao Steven Magoiga kutoka Kampuni ya uwakili ya Kabonde & Maogiga ya jijini Mwanza kwenye kikao ili kupokelewa na kuanza kujadiliwa.

Akitoa ufafanuzi wa kila hoja walizokubaliana na wafanyabiashara hao baada ya majadiliano ya kina na mabishano ya kisheria juu ya tafasiri ya sheria hizo kwa baadhi ya hoja hizo, hoja ya kwanza ya tozo za leseni kuwa na kiwango kikubwa na tofauti tofauti, alisema hili lilikua chini ya Mamlaka ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Hoja hii ilibidi lilizua mjadala mkali lakini ilibidi kuwaonyesha nyaraka za jedwali la tozo za leseni kutoka Wizarani inayoonyesha viwango na tozo za leseni kulingana na madaraja ya biashara kubwa, kati na ndogo ambapo tulikubaliana kuendelea kutozwa kwa kuzingatia viwango hivyo kwa mujibu wa sheria zilivyoainisha,”alisema.

Alieleza kuwa wali tozo hizi ziliondolewa na Wizara lakini hazikusema Halmashauri ziache kutoza tozo za leseni na zimekuwa zikifanya hivyo kulingana na sheria zilizopo kwenye halmashauri hizo ambazo zimekuwa zikitekelezeka tangu mwaka 2000 sheria ilipopitishwa. 

Mkurugenzi Hida akifafanua hoja ya tozo za ushuru wa maegesho ya magari mjini kati ambapo kwa siku na mwezi kuwa kubwa hivyo Jumuiya hiyo ilipendekeza kuondolewa kabisa pamoja na kupitishwa kwa sheria ndogo ya mwaka 2000, alisema tulijadiliana na kuafikiana liendelee lakini tutamuelekeza wakala aliyepewa zabuni hii kutumia busara wakati wa ukusanyaji ili kutokuwa kero kwa wananchi kwani liko kisheria.

“Tulijadiliana kwa kina na sisi kama jiji tukasema ni utekelezaji wa sheria zetu hivyo tumelichukua na tutaliwasilisha na kuanza kulipitia upya katika mchakato wake ili kuliwasilisha kwa utaratibu kwenye vikao vya Baraza la Madiwani wa jiji ili kuona kama lintafanyiwa marekebisho,”alisema.

Aliongeza kuwa ushuru huu wa maegesho kwa sasa hauwezi kufutwa na kuondolewa kwa kuwa ni moja ya vyanzo vya ndani vya mapato vya Halmashauri ambavyo vilipitishwa kisheria na Baraza na kupata Baraka za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo wamelizia.

Hida kitolea ufafanuzi hoja ya kupanda kwa tozo ya gharama za uzoaji taka, ambapo JWT ilitaka kupunguzwa kutokana na kupanda kutoka Sh 8,000 kwa mwezi hadi 15,000 kwa mwezi walijadiliana na kukubaliana kuwa, kutokana na kazi hiyo kufanywa na vikundi vya usafi ambao ndiyo mawakala wa jiji ili kusaidia jiji kuwa safi wamelichukua kuelekeza kwa vikundi hivyo. 

Ufafanuzi ni kwamba tumewaeleza wafanyabiashara kuwa hili tunaliangalia hivyo kwa kipidi tunalifanyia kazi, sasa wataendelea kulipa kiasi cha Sh 8,000 kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2000 iliyolipitisha wakati tukisubili kuwasilisha kwa vikao vya Baraza kulifanyia marekebisho na tunaliangalia kwa upana zaidi ili lisiathili usafi wa jiji.

“Usafi kila mahari ni wajibu hivyo tumekubaliana liendelee kwa kulipa gharama ya Sh 8,000 kuchangia uzoaji taka  ili kulinda hadhi ya Jiji letu kuendelea kuwa safi na kuondoa na kuacha kuchangia hali itakuwa mbaya zaidi wameliona na kuomba waendelee nasi tumekubaliana nao,”alisisitiza.

Mukurugenzia huyo alisema kuwa hoja nyingine ilikuwa ni kuondolewa kwa ushuru wa huduma ya vyoo vya Jiji vinavyotumiwa na umma kwa kulipia ambapo hutozwa Sh 200 (haja ndogo) na Sh 300 (haja kubwa na kuoga), alisema kuwa tumekubali na tutawaelekeza mawakala waliopewa zabuni hizo kutoza Sh 100 (haja ndogo) na Sh 200 (haja kubwa na kuoga).

“Hili nalo ni jambo ambalo tumekubaliana na wafanyabiashara kuendelea kuchangia ili kusaidia usafi katika sehemu hizo za kutolea huduma kwenye vyoo vilivyoko stendi za basi , masoko na maeneo mengine ili kutokuwa na utofauti wakati tukijipanga kutekeleza mkakati wa kuongeza na kuboresha vyoo vingine ili kukidhi mahitajikwa watumiaji,”alisisitiza.

Hida alisema kwamba katika hoja ya kukamatiwa mizigo na magari ikiwemo kufungwa cheni wakati wa kushusha bidhaa kwenye maduka ilizua mjadala mkali na kufikia muafaka ambao kwa mjibu wa sheria ndogo ya mwaka 2010 iliyopitishwa na Halmashauri ya Jiji.

Alifafanua kuwa kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kutumia udanganyifu wa kushusha mizigo lakini kutoingiza kwenye maghala ya kuhifadhia lilipelekea sheria hii kutekelezwa na askari mgambo wa Jiji na wakala wa kukusanya ushuru wa maegesho na kufikia muafaka.

“Tumekubaliana kuwa magari yote ya mizigo ya wafanyabiasha nayohitaji kushusha mjini kati sasa kushusha  kuanzaia saa Jiji tumekubali yashushe kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 12:00 alfajili ili kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara na maeneo hayo ,”alisima.

Alisisitiza kuwa katika makubaliano hayo gari litakalukutwa likishusha mizigo kuanzia saa 2:00 hadi 11:45 litakamatwa kwa kuvunja sheria na makubaliano na askari mgambo na wakala aruhusiwi kukamata au kufunga cheni gari muda ambao wameruhusiwa kushusha.

“Lakini jiji limetoa siku nzima kwa wafanyabiashara kuondosha mizigo yao iliyoshushwa na magari katika maeneo ya maduka yao endapo itabainika kukaa siku mbili hatua kali zitachukuliwa na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria zilizopitishwa,”alisisitiza.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kutekeleza sheria ya kuondosha matoroli na mikokoteni kutoa huduma katikati ya Mji na badala yake Jiji limebaliki kutumika kwa baiskeli za magurudumu matatu, bajaji na gari ndogo aina ya Pikapu ili kusaidia kuondosha msongamano mjini.

Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na uongozi wa jiji katika kutekeleza majukumu ya kila siku ikiwemo utolewaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya kata zote 12 za jiji hili lakini pia akishauri wafanyabiashara kutotumia sehemu ya migomo kama kutaka kutekelezwa kwa hoja na matakwa ya uvunjwaji wa sheria.

“Jiji litaendelea kutekeleza sheria zilizopo ikiwemo za ardhi na mipango miji, usafi na mazingira, usafiri na usafilishaji na zingine na zilizopitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya TAMISEMI,”alisema.

Baada ya kikao hicho kukaa kuanzia majira ya saa 4:00 hadi saa 3:00 usiku juzi kilifikia muafaka huo na kusitishwa kwa mgomo ambapo uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ulitangaza kumalizika na kutoa ruhusa kufunguliwa kwa maduka katikati ya Jiji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.