Nikama msimu wa makombe kwao hatimaye timu ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Mwanza imeibuka washindi katika michuano wa tamasha la msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta Soka Bonanza lillowakutanisha mashabiki wa vilabu vinane vya soka barani ulaya mara baada ya kuwagagadua Chelsea katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.
Washindi wa pili Chelsea moja kati ya timu zilizo onyesha kandanda safi la ufundi wakiongozwa na rais wao Dj Cutter aliyebeba kombe.
M-blogishaji maarufu nchini Tanzania wa blogu ya JIACHIE 'Michuzi junior' jicho kikazi zaidi katikati ya raha na wadau wa Mwanza kulia Muhksin Mambo wa THE BIG TOP TEN na kushoto ni Ramadhani wa Vila park.
Dakika sifuri wala halikuwa tena suala la kujificha kwani kama ni shangwe za mashabiki basi Arsenal ndiyo waliongoza kwani walijipanga bwana! kuna huyu mdau waliye mpachika jina 'TUMBO' alikuwa kivutio kweli kwa kuliongoza jahazi la mashabiki wa timu ya Arsenal katika mashangweZZz!Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment