ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 10, 2025

GAMONDI ATEMA MAJINA MAKUBWA STARS KUELEKEA AFCON 2025.

 

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Miguel Gamondi, ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoiwakilisha nchi katika fainali za AFCON 2025 zitakazofanyika nchini Morocco.

Taifa Stars imepangwa kwenye Kundi C, pamoja na timu ngumu kama Nigeria, Tunisia na jirani zetu Uganda (The Cranes).

Miongoni mwa mastaa waliopata nafasi kwenye kikosi hicho ni Nahodha Mbwana Samatta, Simon Msuva, Kibu Dennis na Kelvin John, ambao wataongoza safu ya ushambuliaji ya Stars.

Hata hivyo, katika sura mpya za uchaguzi wa kikosi, mfungaji kinara wa Ligi Kuu Bara Paul Peter (magoli 5), mshambuliaji wa Simba SC Selemani Mwalimu, pamoja na kiungo wa Yanga Mudathir Yahya hawajapata nafasi, jambo lililozua mijadala kutoka kwa mashabiki.

Kikosi hiki kinatarajiwa kuingia kambini hivi karibuni kwa maandalizi ya michuano hiyo mikubwa ya bara Afrika.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment