ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 15, 2025

MAANDALIZI KABAMBE YA JUKWAA LA 4 LA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Katika kuelekea Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, CPA. Venance Kasiki, amefafanua umuhimu, malengo na matarajio ya jukwaa hilo litakalofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 16 hadi 18 Juni, 2025.
CPA. Kasiki amesema lengo kuu la jukwaa hilo ni kutoa fursa kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa madini kupitia huduma na bidhaa wanazoweza kutoa kwenye mnyororo wa thamani ya madini. Ameeleza kuwa, jukwaa hilo pia litaweka mkazo kwenye ushirikiano kati ya serikali, wawekezaji na watoa huduma wa ndani, huku likipambanua fursa mpya zinazopatikana ndani ya sekta hiyo.

Jukwaa hilo litahusisha maonyesho, mijadala ya kitaalamu, mikutano ya kibiashara na majadiliano ya sera ili kuhakikisha Watanzania wanajumuishwa ipasavyo na kunufaika zaidi na utajiri wa rasilimali za madini nchini.






Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment