ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 22, 2025

INTER MILAN YATOKA NYUMA NA KUICHAPA URAWA RED DIAMONDS 2-1 MAREKANI

 

TIMU ya Inter Milan ya Italia jana ilitoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Urawa Red Diamonds ya Japan katika mchezo wa Kundi E Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA Uwanja Lumen Field, Seattle, Washington, Marekani.


Winga Ryōma Watanabe alianza kuifungia Urawa Red Diamonds dakika ya 11, kabla ya mabao ya Waargentina wawili kubadili mambo – kwanza mshambuliaji Lautaro Martínez akiisawazishia Inter Milan dakika ya 78 na kiungo Valentín Carboni kufunga la ushindi dakika ya 90’+2.


Mechi nyingine ya Kundi E jana River Plate ya Argentina ilitoka sare ya bila mabao na Monterrey ya Mexico Uwanja wa Rose Bowl, Pasadena.


Baada ya matokeo hayo, sasa River Plate inaongoza Kundi E kwa pointi zake nne ikiizidi tu bao moja Inter Milan, wakati Monterrey yenye pointi mbili inashika nafasi ya tatu na Urawa Red Diamonds inaburuza mkia kufuatia kupoteza mechi zote mbili za mwanzo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment