![]() |
| Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akitoa neno la ufungua wa Tamasha la pili la JEMBEKA FESTIVAL. |
![]() |
| Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba, Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula pamoja na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye wakimsikiliza Dr. Sebastian Ndege ( pichani chini). |
Licha ya msanii NE-YO pia kulikuwapo na wasanii wa nchini wakiongozwa na Diamond Platinumz ambaye aliambatana na timu yake kutoka lebo yake ya Wasafi (WCB), wasanii wengine ni Fid Q, Baraka Da Prince, Ney wa Mitego, Maua Sama, Mo Music, Stamina, Juma Nature a.k.a Kiroboto, Ruby na wengine wengi.Tamasha hilo lilifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo pia lilihudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye na Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba pamoja na Mwanamitindo wa Kimataifa nchini, Flaviana Matata ambao kwa pamoja walionekana kufurahia tamasha hilo la kihistoria kuwahi kufanyika jijini Mwanza.
Kufanyika kwa tamasha hilo kulisimamiwa na mikono ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu, Coca Cola, FastJet, SYSCORP, EF Outdoor, Ndege Insurance Brokers, Jembe FM, Double Tree, KK Security na Mo Entertainment ambao ndiyo waliowezesha kufanyika kwa tamasha hilo.
Tupe maoni yako


















0 comments:
Post a Comment