Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda, leo anatarajiwa kuzuru jijini Mwanza kwa ajili ya kuendesha harambee ya kuchangisha sh. Bilioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando inayoadhimisha miaka 40 tangu ilipoanzishwa rasmi mnamo mwaka 1971.Akithibitisha kuhusu ujio wa kiongozi huyo wa kiserikali Mkurugenzi wa Hospitali ya bugando Dk Charles majinge amesema fedha hizo zitatumika kujenga maabara ya Saratani hospitalini hapo ambayo inatajwa kuleta mapinduzi ya utabibu nchini pindi itakapokamilika.
Kwamujibu wa Mkurugenzi huyo wa Hospitali ya Bugando harambee hiyo itafanyika leo kuanzia saa moja kamili jioni katika ukumbi wa Hotel Gold Crest iliyopo katikati ya jiji la Mwanza.
Akifafanua zaidi Dr. Majinge amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo unamatumaini kwamba malengo ya makusanyo yaliyokadiriwa yatafikiwa sanjari na kuzidi malengo yaliyotajwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment