ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 9, 2017

WATU 12 WAFARIKI DUNIA BAADA YA DALADALA KUPITILIZA ZIWANI VICTORIA.

YALIYOJIRI MZ HII LEO:- Gari lilipoteza breki kutoka mbali na gari zinazofanya safari kati ya Kigongo na Buhongwa, ndani ya yard hapakuwa na gari lolote hivyo dreva akapitiliza moja Kwa moja hadi majini ziwani!!! #JembeHabari

“Kwa mshtuko na masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha baada ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika ziwa Victoria Mkoani Mwanza, nawapa pole sana wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hii, nawaomba wawe na moyo wa uvumilivu,ustahimilivu na subira katika kipindi hiki cha majonzi”.

Hiyo ni sehemu ya salamu za rambirambi alizozitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella kufuatia ajali ya basi la abiria (Daladala) lililozama katika ziwa Victoria baada ya kugonga vizuizi vya kivuko cha Kigongo Wilayani Misungwi na kisha kutumbukia na kuzama majini.

Mhe.Rais Magufuli amemtuma Bw.Mongella kufikisha salamu zake za pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki wote waliopatwa na msiba huu na amesema anaungana nao katika maombolezo.

Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi na majeruhi 3 walionusurika katika ajali hii wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.