ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 15, 2015

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA AKUTANA NA VIJANA WA SOKA WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU MWANZA

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kushoto) akikabidhi msaada wa jezi na bukta zake kwa mtoto Sunday Hassan ambaye alisimama kwa niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaosimamiwa na kituo cha kulea na kukuza vipaji vya soka cha TSC Academy cha jijini Mwanza, kulia ni Rais wa TSC Altaf Hirani ambaye pia ni Mkurugenzi wa MOIL akifanya usaidizi kwa makabidhiano.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose amesema kuwa shughuli za kusimamia watoto wanao taabika wakiishi kwenye mazingira magumu ni muhimu sana kwa jamii yote kwani watoto hao wakikosa misingi mizuri kama elimu, maadili, chakula, afya na makazi ya kueleweka wanaweza kuwa na madhara makubwa kwa Taifa.

Hivyo amewataka Watanzania wazalendo na wale wageni wenye mapenzi mema, vituo mbalimbali, makampuni na watu binafsi kuitikia wito kwa kuwasaidia watoto hao katika kufanikisha ndoto zao.

Wakisikiliza kwa umakini (walioketi) hawa ni baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaosimamiwa na kituo cha kulea na kukuza vipaji vya soka cha TSC Academy cha jijini Mwanza.
Wakisikiliza kwa umakini huku wengine wakichukuwa kumbukumbu.
Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wenye umri wa chini ya miaka 12 wanaosimamiwa na kituo cha kulea na kukuza vipaji vya soka cha TSC Academy cha jijini Mwanza, wakijumuika kwenye mazoezi chini ya kocha wao Nyangi Kilacha.
Kocha Nyangi Kilacha akitoa maelekezo kwa timu ya vijana wa chini ya miaka 14 ambao ni sehemu ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaosimamiwa na kituo cha kulea na kukuza vipaji vya soka cha TSC Academy cha jijini Mwanza, waliojumuika kwenye mazoezi hii leo na kuupokea ubalozi wa Uingereza uliowatembelea. 

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose akiwa na Rais wa TSC Altaf Hirani aka Dogo ambaye pia ni Mkurugenzi wa MOIL katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu mabingwa wa Kombe la Dunia la vijana wa mitaani TSC Academy waliolinyakuwa mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil 2014.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose na TSC.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose katika picha ya pamoja na golikipa bora wa mabingwa wa Kombe la Dunia la vijana wa mitaani TSC Academy waliolinyakuwa mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil 2014.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose akiwa na Rais wa TSC Altaf Hirani aka Dogo ambaye pia ni Mkurugenzi wa MOIL katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu mabingwa wa Kombe la Dunia la vijana wa mitaani TSC Academy waliolinyakuwa mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil 2014.
Licha ya kuishi katika mazingira ya ushawishi na hatarishi katika malezi, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose amesihi vijana hao kuzingatia mafunzo wanayopewa yakiwemo yale ya kuishi  na kumjua Mungu huku wakijiepusha na vishawishi vitakavyo waingiza katika majaribu yanayoweza kufifisha ndoto zao za mafanikio.

Ili kuweza kukuza vipaji na kuwa na mfumo endelevu wa kuendeleza vijana hao ambao watakuwa na manufaa na mabadiliko chanya kwa taifa katika medani ya mchezo wakandanda nchini 
Rais wa TSC Altaf Hirani aka Dogo amesema kuwa endapo Serikali ya mkoa wa Mwanza itatimiza ahadi yake ya kukipatia kituo hicho eneo la michezo kama ahadi yake maendeleo makubwa katika mchezo wa soka yatapatikana.

"Mwaka jana tuliporudi toka Brazil tukiwa mabingwa wa Kombe la Dunia la vijana waishio Mazingira magumu, katika sherehe aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Injinia Evarist Ndikilo pamoja ofisi ya Halmashauri ya jiji kupitia Meya wake Stanslaus Mabula waliahidi kutupatia eneo ambalo litatumika kujenga kituo cha michezo ahadi ambayo mpaka sasa bado haijatekelezwa lakini ninaimani Serikali haitotuangusha kwa hili na nina imani watatupa sapoti ya kutosha" 

"Katika kutimiza ndoto zetu sisi kama kituo tayari tumeshakamilisha taratibu zote za awali kwani tumeshapeleka barua kwa Halmashauri husika, hivyo kikubwa tunasubiri majibu kutoka kwao kwani wawekezaji toka nje wameonyesha nia ya kutusaidia na wapo tayari kwa ajili ya mpango wa ujenzi wa kituo hicho cha michezo" Alisema 
Altaf Hirani.  

Albert G. Sengo
albertgsengo@yahoo.com
+255 754 074 152

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.