Katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru maelfu walifurika kwa ajili ya kutambua jamaa zao ambapo mke na mume ambao ni Elly Kaaya, Ofisa Elimu na Kumbukumbu wa Halmashauri ya Meru na mumewe Kundaeli Kaaya ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Ndoombo wilayani Arumeru walikuwa ni miongoni mwa maiti zilizotambulika katika ajali hiyo.
Tukio hiilo limetokea jana eneo la Madila kwenye Kijiji cha Sing’isi saa 11 jioni baada ya gari hilo la abiria lililokuwa linatokea Usa River kwenda Arusha kugongana na lori hilo lililokuwa linatoka Arusha kwenda Kilimanjaro.
Wengine waliotambuliwa katika ajali hiyo ni pamoja na Ofisa Elimu wa Taaluma Halmashauri ya Meru, Zakia Katunga na kondakta wa gari hilo, Simon Wilenya na abiria Kundaeli Kadoya.
Hadi jana jioni, miili mingine sita ilikuwa bado haijatambulika, huku mamia ya watu wakiendelea kufika katika uwanja wa chumba cha kuhifadhi maiti kutambua miili hiyo.
Hata hivyo, hadi jana dereva wa gari la abiria alikuwa hajulikana alipo na majeruhi wengine watatu walikuwa wamelazwa wakiwa mahututi Hospitali ya Wilaya ya Meru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kesho (leo) angetoa taarifa ya tukio hilo.
Jaji Luhangisa aliteuliwa hivi karibuni, kuwa Jaji na Rais Jakaya Kikwete.
Hiace hiyo kwa upande wa mbele. |
Polisi wa usalama barabarani wakisimamia zoezi la kuiondosha Hiace hiyo kwenda kuhifadhi mahali stahili. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.