Polisi walionekana kutanda kwenye maeneo mbalimbali jijini hapa wakiwa na silaha za moto, huku gari la maji ya kuwasha nalo likipita mitaa kadhaa ya barabara muhimu kuashiria kuwasaka waandamanaji.
|
POLISI mkoani Mwanza wamewatia mbaroni viongozi sita na wafuasi kadhaa wa CHADEMA waliokuwa wakijiandaa kuandamana ikiwa ni hatua mara baada ya wanachama hao kukaidi amri ya polisi iliyowekwa ya kusitisha maandamano.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 5.20 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao kujipanga kuanza maandamano yaliyokuwa yaanzie Viwanja vya Sahara mkoni Mwanza hadi Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana zilizopo katikati ya na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
Katika purukushani hiyo iliyodumu zaidi ya masaa mawili huku ikiambatana na wafuasi hao kupigwa virungu, Polisi wamewatia mbaroni watu takribani 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Aidha Polisi walionekana kutanda kwenye maeneo mbalimbali jijini hapa wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi huku gari la maji ya kuwasha nalo likipita mitaa kadhaa ya barabara muhimu kuashiria kuwasaka waandamanaji.
Licha ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado halijatoa taarifa kamili na idadi ya watu inayowashikilia.
Polisi wakipita katika mtaa wa Kemondo na Nyerere kufanya doria kufuatia taarifa za maandamano ya CHADEMA kutangazwa jijini Mwanza. |
Polisi katikati ya mji wa Mwanza wakifanya doria. |
Ingawa kuna ukimya lakini kuna taarifa za kichini chini zikisema, Inasemekana waandamanaji watatumia style tofauti kukusanyika kwenye ofisi mbili walizozitaja, moja wapo ikiwa ni Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wakitoka pande mbalimbali za mji. |
Polisi wakiwashusha kituoni baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliowakamata. |
Hatua kwahatua. |
Mpaka ndani. |
Katibu wa Baraza la Wanawake Wilaya ya Ilemela CHADEMA akizungumza na waandishi wa habari amesema bado maandamano yataendelea na hayatokoma mpaka ujumbe utakapofika kama ilivyokusudiwa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA. |
Katibu Mkuu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza John Nzwalile amesema kuwa maandamano yao yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani polisi wameshiriki kwa kuwa na idadi kubwa kuandamana wakitapatapa kwenye mitaa mbalimbali kuwasaka wananchi ambao hawana silaha kama wao. Wananchi wazalendo wanao andamana kwa amani kufikisha ujumbe kwamba kuna mamilioni yao yanaliwa na Bunge la kataba ambalo halina dalili yoyote kutoa matokeo ya katiba mpya inayohitajika kwa watanzania, huku akihoji kwa nini fedha hizo zisilipe waalimu na madaktari wenye madeni yao?...!! ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA |
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali wakiwa katika moja ya kona ya barabara kuchukuwa matukio. |
Msako ukiendelea. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.