ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 24, 2013

BASI LA MOHAMED LAACHA NJIA.

Basi la Mohamed linalofanya safari zake kutoka Mwanza kuelekea Bukoba limeacha njia na kuvamia mashamba yaliyopo pembezoni mwa barabara asubuhi ya leo. 
Kwa mujibu wa mpenyezaji wa taarifa hizi ambaye alikuwa akipishana na basi hilo amesema kuwa hakuna abiria yeyote alipoteza uhai wala aliyejeruhiwa zaidi ya abiria kadhaa kujawa hofu. 
Mpaka mpenyezaji wa taarifa hii anatoka eneo la tukio matairi ya basi hilo yalikuwa yamezama kwenye tope huku juhudi za kuliondosha basi hilo kurejea barabarani zikifanyika. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.