ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 1, 2018

MAAMUZI YA SERIKALI KUONGEZA UZALISHAJI WA UMEME YAENDE SANJARI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA- DKT KALEMANI


NA AMIRI KILAGALILA/GSENGOtV

NJOMBE

Waziri wa Nishati DK.MEDARD KALEMANI amewataka Viongozi na wadau wa nishati kuwasaidia wananchi hususani wakazi wa mkoa wa Njombe kutunza vyanzo vya maji ili kuwezesha ukuzaji wa mto kilombero unaolisha maji yake mto Rufiji maalumu kwa mradi wa kuzalisha umeme wa rufiji wenye uwezo wa kuzalisha umeme takribani MW.2,1OO.

Waziri KALEMANI ameyasema hayo wakati wa mkutano wa uelewa wa mradi wa kuzalisha umeme wa rufiji (rufiji hydropower project) uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ulio wakutanisha wadau mbali mbali wakiwemo wabunge na  viongozi wa halmashauri za mkoa wa Njombe.



Aidha dk.kalemani amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imeamua kutekeleza mradi huo mkubwa wa mda mrefu ulionza kubuniwa tangu serikali ya awamu ya kwanza na leo umeanza kutekelezwa ukiwa na zaidi ya miaka 40 huku sababu kubwa ikiwa ni kuongezeka kwa matumizi makubwa ya umeme nchini.

Kalemani ameongeza kuwa licha ya hali ya umeme kwa sasa kuwa bora kwa kuwa na umeme wa ziada megawati 201 lakini haiwezi kutoshereza katika mahitaji ya uchumi wa viwanda ndio maana serikali imeamua kuongeza uzalishaji wa umeme mwingi na wakutosha  ambao ghalama yake ni naafuu licha ya serikali kuendelea kuzalisha umeme mchanganyiko ukiwemo wa gesi. 

Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe ALLY KASINGE licha ya kupongeza jitihada za kuanza mradi huo mkubwa wa umeme nchini, amesema kuwa ikiwa Njombe ni miongoni mwa mikoa yenye vyanzo vingi vya maji yanayolisha mto rufiji wanayosababu ya kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa vyanzo hivyo vya maji ili kusadia juhudi za wizara katika kufikia umeme wa kutosha kuelekea uchumi wa viwanda.

MAADHIMISHO YA WIKI YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KITAIFA YAFUNGWA JIJINI DODOMA.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye, akitoa taarifa ya Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi toka Makao Makuu wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, jinsi wanavyoweza kufanya maokozi kwenye majengo marefu pindi ajali inapotokea, alipotembela Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini humo jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, akipokea zawadi ya kizimia moto cha awali (Fire Extinguisher) kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto Philibert Chaki, alipotembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini Dodoma jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akimkabidhi cheti mwakilishi wa TCRA, ambaye jina lake halikupatikana kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyoanza Agosti 29, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi ya kikombe Konstebo wa Timu ya Polisi Dodoma, Ally Juma mara baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja dhidi ya wapinzani wao Timu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini Dodoma jana.
Msanii Mrisho Mpoto na kundi lake wakitumbuiza wimbo maalum wenye maudhui ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji, mbele ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana. (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola (Mb) Agosti 29, 2018 katika Uwanja cha Jamhuri Jijini Doodma na kufungwa jana Agosti 31, 2018 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa mwaka huu ni “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA KUFUNGA VING’AMUAMOTO VIWANDANI”

TANZANIA IS A RESOURCE BLESSED OR RESOURCES CURSE?


Edwin  Soko
Independent Journalist

Tanzania  is  a  resource   blessed   or  resources  curse ?
A country’s mineral wealth should be a blessing for its people. However, experience in various countries has shown that the endowment with mineral wealth can prove to be very problematic instead – a phenomenon known as the “resource curse”.
In recent years, discovery and exploitation of minerals in Eastern Africa has rapidly expanded. This raises questions and concerns about their impact on the future of the region.
Program    manager    from  governance   link  Mr. Pentalione   Shoki,  said  that,  Tanzania is a relatively late arrival to large-scale mining, the history and current status of discovery and exploitation of mineral resources in Tanzania, about the socio-economic implications, and about the legal and political framework in which mining in Tanzania operates.
Shoki  added    that, if timely investments are made in promoting and implementing good practices in the mining sector, the problems that have plagued other resource-rich countries can be avoided in East Africa.
Tanzania   is  a land   rich   in minerals, mining   makes  up   more  than 50% of  the  country’s total   export   of  which   a  large   part  comes   from  gold,  The  country   has   gold   reserves  of  45  million  ounce, generating   revenue   of  over   a  billion USD.  Diamond  are  also   found   in significant   amounts, since   it was   opened in 1940.
William   diamond   mine  has  produced  19 million  carats (3.800) of  diamond,  Gemstones, nickel, copper, uranium, ka0lin, titanium, cobalt and  platinum  are  also mined  in Tanzania.
Apart  from having  resources   blessed but  the    Tanzanian’s government  has  role to  perform  on deciding  whether   Tanzania  is  resources   blessed  or  resource   course

KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MI-3 YA UBUNGE JIMBO LA BUCHOSA UTAWALA WA SERIKALI AWAMU YA 5 YA JPM, TIZEBA ANA NINI?



GSENGOtV

AFYA:- Huduma ya upasuaji sasa inafanyika katika hospitali za visiwani .
- Jumla ya Zahanati 28 zinajengwa kwa mpigo.

MAJI:- Fedha bilioni 27 kutumika katika ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Jimbo la Buchosa, mradi utakaoanza mapema mwezi Januari 2019.

UMEME:- Tayari umeme umeingia visiwani - Matarajio kufikia 2020 Upatikanaji wa umeme Jimbo la Buchosa utakuwa asilimia 90.

KILIMO:- Buchosa peke yake msimu wa kilimo 2017-2018 ilizalisha pamba kilo laki 465,000, safari hii msimu wa mauzo ukiwa bado unaendelea tayari wamekwisha uza kilo milioni 1,700,000 za pamba, ikiwa ni ongezeko karibia mara nne ya uzalishaji wa msimu uliopita wa mwaka jana 2017.

DKT. BASHIRU ASEMA MIKATABA UWEKEZAJI CCM YA-KIFISADI.





Katibu  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema mikataba ya uwekezaji katika chama hicho na jumuiya zake, inatarajiwa kupitiwa upya kwa kuwa baadhi ni ya kifisadi na kitapeli.

Dk,. Bashiru alisema hayo jana jijini hapa wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), huku akibainisha kuwa umoja huo ndio unaoongoza kuwa na mikataba mingi mibovu.

Alisema lengo la kuipitia upya mikataba hiyo ni kujadiliana kwa misingi ya usawa na hakutakuwa na mkataba ambao chama au jumuiya inapoteza umiliki wake.

Aidha, alisema limeshaundwa baraza la wadhamini wa chama ambalo kwa mujibu wa Katiba ya CCM, lina mamlaka ya kusimamia mali zote za chama na jumuiya zake.

“Yale yote mabaraza ya Jumuiya yaliyokuwapo yalikuwa uchochoro wa wizi na uporaji wa mali za jumuiya na yamefutwa kikatiba,”alisema.

Dk. Bashiru alisema wakati wa uhakiki wa mali za chama kuna mambo yalionyesha kuwa jumuiya hiyo imeanza kupoteza misingi ya nidhamu.

“Mali zenu nyingi zimekuwa hazitumiki vizuri. Ni jumuiya ambayo ina mikataba mibovu na hasa mkataba wa mradi wenu mkubwa pale Dar es Salaam, ni mkataba wa wizi, wa kitapeli,” alisema.

Alibainisha kuwa, chama kimedhamiria kuchukua taratibu za kisheria kurejea mikataba hadi ifike mahali ambapo mwekezaji na umoja huo wanakuwa sawa.

“Hatutaki mikataba ambayo chama au jumuiya inapoteza umiliki wake kama yaliyopo pale kwenye miradi yenu jijini Dar es Salaam. Mikataba ile pamoja na mambo mengine mmepoteza haki ya kumiliki wa ardhi yenu,” alisema.

Alifafanua kuwa, katika moja ya mikataba mwekezaji ametumia hati kukopa na kwamba mkataba huo UVCCM inapata asilimia 25 huku mwekezaji asilimia 75.

“Sasa kwa nini msifanye kama Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wao wameenda kukopa halafu wanajenga halafu watalipa kutokana na uwekezaji waliopata,” alisema huku akisisitiza kuwa: “Mikataba ya aina hiyo imefika mwisho na haitatokea mikataba tena kama hiyo.”

Katika hatua nyingine, Dk. Bashiru aliwataka vijana kuendesha mijadala inayohusu demokrasia katika mitandao ya kijamii ili kuimarisha uhuru wa kujitawala, amani na utulivu.

Aidha, aliwataka viongozi wa UVCCM kuhakikisha wanafanyia kazi suala la ukomo wa madaraka ndani ya jumuiya hiyo kwa kuondoa viongozi au kutochagua viongozi ambao umri wao kikanuni hauruhusiwi.

Akimkaribisha Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Umoja huo, Kheri James, aliwataka wajumbe wa kikao hicho kuchagua watu wenye sifa na uzalendo ndani ya chama na si kuchagua watu ambao ni vibaraka.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Raymond Mwangwala, alisema tangu Katibu Mkuu wa chama aanze kazi sasa ni siku 100 na kwamba amefanya mapinduzi na mabadiliko makubwa ndani ya chama.

Aliwataka vijana hao kuhakikisha wanatetea maslahi ya chama na taifa kwa ujumla badala ya kujikita kwenye mitandao ya kijamii na kwamba wawe mstari wa mbele kumtetea Rais John Magufuli kutokana na utendaji anaofanya.

DAKIKA 5 ZA MHE. NGELEJA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU



GSENGOtV
Huyu hapa Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe. William Ngeleja.

MAKONTENA YA MAKONDA YAKOSA WATEJA TENA.


MNADA wa makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, umefanyika leo Jumamosi, Septemba 1, 2018 katika Bandari ya Dar, lakini imeshindikana kupatikana mnunuzi, hivyo mnada huo utaendelea Jumamosi ijayo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Scolastika Kevala, amesema hawajapata mnunuzi wa kontena hata moja lakini wamefanikiwa kuuza bidhaa 10 tu zilizokuwemo kwenye makontena hayo.

Sehemu kubwa ya bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama vile viti, meza na makabati na vitu vingine.

“Mpaka sasa tayari tumefanya mnada wa makontena yote 20 lakini hayajapata mteja ingawa tumefanikiwa kuuza bidhaa 10 zilizokuwemo kwenye makontena hayo. Hivyo mnada wa makontena utaendelea tena Jumamosi ijayo,” amesema Kevela.

Itakumbukwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango aliagiza makontena hayo kupigwa mnada licha ya RC Makonda kutoa vitisho kuwa atakayenunua vitu vilivyomo kwenye makontena hayo atapata laana.

Aidha, mnada wa makontena hayo unakuja ikiwa ni baada ya Makonda kushindwa kuyalipia kodi kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2.

Friday, August 31, 2018

ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MWANZA - MONGELLA ATOA RATIBA KAMILI.



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

"Mhe. Rais atashuhudia utiaji saini mikataba ya ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli za MV. Butiama, hafla itakayofanyika katika eneo la Bandari ya Kusini (Mwanza South Port) iliyopo kata ya Igogo, Jijini Mwanza tarehe 03 September 2018 kuanzia saa 1:30 Asubuhi"....Ni sehemu ya maelezo ya ziara hiyo.

UDUGU WA JIJI LA WURZBURG NA JIJI LA MWANZA WAZIDI KUNOGA


NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Watanzania wameaswa kuwa na desturi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ili kuona na kujifunza mambo mbalimbali hususani mazingira, wanyama waliopo kwenye hifadhi zote na hata jiografia ya nchi.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Jiji la Mwanza Dkt. Elirehema Kaaya wakati akiwatembeza wageni kutoka Jiji la Wurzburg toka nchini Ujerumani waliofika Jijini Mwanza kutembelea na kufanya utalii kwa jiji hilo lenye urafiki na jiji walilotoka.
Wageni hao wameonekana kuvutiwa na majengo yaliyoachwa na ndugu zao zama za ukoloni sanjari na kustaajabishwa na maandhari nzuri ya miamba ya kuvutia katika jiji la Mwanza.
"Unaweza ukamuuliza mtanzania mwenzangu hii leo, Ni mbuga gani ya wanyama anayoifahamu akabaki kumangamanga asijue la kujibu, ile hali iko kilometa chache kutoka mji anao ishi lakini tizama ndugu zetu hawa wametoka maelfu na makumi ya maili na kilomita kwa nia tu ya kutembelea vivutio vyetu, hii ni aibu kwa wazawa wenzangu, tubadilike" alisema Dkt. Kaaya 
UTALII WA NDANI NI NINI?
Utalii wa ndani ni kule kutembea kutoka mahali pamoja hadi pengine ndani ya nchi husika. Tabia ya watu kuthamini na kufanya utalii wa ndani inaweza kuchochewa kwa kuwapo sera za utalii wa ndani kuanzia ngazi ya shule, vyuo, taasisi za dini na katika ofisi mbalimbali za umma na binafsi.
Shule na vyuo zina nafasi kubwa ya kuhamasisha kwa sababu zenyewe ni mojawapo ya wakala mkubwa wa mabadiliko na maendeleo katika jamii. Kwa mfano, ni watu wangapi wanaofahamu kuwa kuna aina rahisi ya utalii wa kufanywa kwa kutumia baiskeli?
CHUNGULIA KIDEO.

MAANDAMANO MAKUBWA YASHUHUDIWA KAMPALA NCHINI UGANDA BAADA YA MBUNGE BOBI WINE KUKAMATWA TENA.

Maandamano yashuhudiwa Kampala, Uganda baada ya Mbunge Bobi Wine kukamatwa tena




Mji mkuu wa Uganda Kampala, leo umeshuhudia malalamiko na maandamano baada ya polisi kuwatia mbaroni wabunge wawili wa upinzani wakiwa katika harakati za kuelekea nje ya nchi kwa matibabu.

Wabunge wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine na Francis Zaake walitiwa mbaroni jana usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe wakiwa katika pirikapirika za kutaka kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Wakili wa mbunge Bobi Wine amesema kuwa, mteja wake alizuiwa kuingia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe na kuchukuliwa na polisi ambao wanadaiwa kumpeleka katika hospital ya serikali. 
Maandamano ya leo ya wafuasi wa wabunge hao yameshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Kampala ambapo waandamanaji wenye hasira waliweka vizuizi barabarani na kuchoma moto matairi.

Vikosi vya usalama vilikuwa na kazi ya ziada kuzima maandamano hayo na kusafisha barabara zilizokuwa zimejaa vizuizi. 
Mbunge Bobi Wine ambaye amejizolea umashuhuri mkubwa hivi karibuni nchini Uganda anakabiliwa na makosa ya uhaini, kufuatia tukio la kushambuliwa kwa mawe gari la Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni katika kampeni za uchaguzi mdogo huko Arua.  Bobi Wine aliachiliwa kwa dhamana kutoka kizuizini alikokuwa akishikiliwa siku ya Jumatatu, akiwa katika hali mbaya kiafya.
Ripoti mbalimbali zinasema kuwa, wabunge hao akiwemo Bobi Wine waliteswa vibaya wakati walipokuwa kizuizini, ingawa serikali ya Kampala kupitia msemaji wake Ofwono Opondo ilisisitiza tena wiki iliyopita kwamba, taarifa za kuteswa wabunge hao ni za uwongo.

HIVI NDIVYO MWENGE WA UHURU ULIVOPOKELEWA WILAYANI NYAMAGANA MKOANI MWANZA


NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Hatimaye Mwenge wa Uhuru asubuhi ya leo tarehe 31 Agosti 2018 umepokelewa wilayani Nyamagana ukitokea wilaya za Sengerema na Buchosa ambako umekimbizwa ukikagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo. Fuatilia video hii kuona yapi yaliyojiri.

MWENGE WA UHURU WATINGA JIJINI MWANZA.

NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
PICHANI JUU:- Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Mhe. Dkt. Philis Nyimbi akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipole baada ya kumaliza mbio zake wilayani Sengerema na Buchosa.
Miradi itakayopitiwa na mbio za Mwenge kwa Halmashauri ya jiji la Mwanza ina thamani ya shilingi bilioni 4.8.
Katika eneo la Kamanga Feri jijini hapa, mapokezi yamefanyika mapema leo asubuhi ambapo Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Injinia Charles Francis Kabeho ametumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi na walezi kutimiza wajibu wao kwa kuwapa mahitaji muhimu ya shule watoto wao katika kipindi hiki ambacho serikali inatekeleza mpango wa elimu bure ili kuwawezesha kupata elimu bora.

Aidha ameonya kuhusu suala la dawa za kulevya kwa vijana ambapo amewataka kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa yanahatarisha maendeleo ya taifa na kuwahimiza kuwa wazalendo.
Hatua kwa hatua za makabidhiano.

Mwenge wa Uhuru mikononi mwa Mbunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula.

Mwenge wa Uhuru mikononi mwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Mhe. Kiomoni Kibamba.




Ngoma asili.

Thursday, August 30, 2018

"SINA BIFU NA MEYA WA JIJI LA MWANZA" ASEMA MKURUGENZI KIOMONI KIBAMBA


GSENGOtV
"Mimi na Meya ni marafiki"
"Ni rafiki yangu, tuko vizuri"
"I wish siku moja tuje naye hapa" 

Ni kauli ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba akijibu swali la mtangazaji wa kipindi cha KAZI NA NGOMA toka Jembe Fm, Mansour Jumanne, wakati akitoa ratiba ya mbio za Mwenge wa Uhuru hii leo, unaotarajiwa kuingia katikati ya Jiji la miamba (Mwanza) Kesho tarehe 1 Mwezi September 2018 kukagua na kuzindua miradi mbalimbali iliyo chini ya mipango ya utekelezaji wa ilani ya CCM kupitia fedha za Serikali.

Ikumbukwe mnamo October 30 mwaka jana 2017 Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire alikamatwa na jeshi la Polisi, na kuswekwa ndani saa chache kabla ya Mhe. Rais John Magufuli kutua jijini hapa kwa ziara, huku kukiwa na sintofahamu ya mahusiano na mvutano kati yake na Kibamba ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji, na ikasemekena kuwa Mkurugenzi ni mmoja kati ya watu walioinjinia mpango huo wa kumweka nyuma ya nondo. 

MASWALI MENGINE ALIYOJIBU
- Hana shaka na miradi ya inayokwenda kuzinduliwa/kukaguliwa na Mwenge 2018

- Vipi kuhusu mikopo na taratibu zake jeh anasema nini juu ya shutuma kwamba ipo kwaajili ya kukifeva wadau wa chama tawala pekee?

- Fununu za yeye kuwania nafasi za siasa chaguzi zijazo hususani UBUNGE Jeh ni kweli?

- Kafunguka pia kuhusu kuirudisha hadhi na heshima ya usafi ya Jiji la Mwanza kitaifa na Kanda ya Afrika Mashariki.

- Mkurugenzi wa Jiji ndiye Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Wilaya, Jeh unaweza kuwatangaza wapinzani kuwa ni washindi pindi pale watakaposhinda?

MAKUNDI YA UEFA YATOKA, LIVERPOOL YAPANGWA KUNDI LA KIFO.

Ratiba ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imetoka jioni ya leo huku ikimshuhudia bingwa mtetezi, Real Madrid ikipangwa kundi moja na AS Roma, CSK Moskiva pamoja na Plazen.

Timu za England, Liverpool ipo kundi la kifo sambamba na Napoli, PSG na Crvena huku Manchester United ikijiandaa kukabiliana na nyota wake wa zamani Cristiano Ronaldo akiwa na klabu yake mpya ya Juventus.

Tottenham Hotspurs wamepangwa kundi B wakiwa na Bracelona, Inter Milan na PSV.



JPM ATAJWA KUWA MGENI RASMI TAMASHA LA URITHI.

RAIS John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama Urithi Festival, Celebrating Our Heritage litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema lengo la Tamasha  hilo  ni kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.

Aidha, Amesema kwa kutambua hazina kubwa ya malikale na utamaduni wa makabila zaidi ya 128 yaliyopo nchini, tamasha hilo litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kukuza utalii wa utamaduni wa malikale hatua ambayo itaongeza ushindani wa Tanzania kama kituo bora cha utalii kwenye masoko mbalimbali duniani.

Ameongeza kuwa Urithi  Festival itasadia kukuza utalii wa ndani kwa kuongeza muda wa watalii wa kimataifa kukaa nchini kwa vile Tamasha hilo lifanyika katika kipindi ambacho watalii wengi wanatembelea Tanzania.

RAIS DKT. MAGUFULI APIGILIA MSUMALI MAKONTENA YA MAKONDA.


 GSENGOtV
Kwa mara ya kwanza Rais John Magufuli ameliongelea sakata la makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda yaliyozuiliwa bandarini na TRA yakitakiwa kulipiwa ushuru kama ambavyo sheria inaelekeza.

MCHEZAJI BORA ULAYA KUJULIKANA LEO.



GSENGOtV
Tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa Ulaya (UEFA) msimu wa 2017/18 inatarajiwa kutolewa usiku wa leo mjini Monaco nchini Ufaransa ambapo majina matatu yanayowania tuzo hiyo ni Cristiano Ronaldo wa Juventus, Mohamed Salah anayechezea Liverpool na Luka Modric wa Real Madrid.

Tuzo hiyo imevuta hisia kubwa ya mashabiki wa soka kutokana na namna kila mchezaji alivyopambana kuisaidia klabu yake kwa msimu mzima uliomalizika. Hapa tunakuletea uchambuzi wa kila mchezaji kuelekea tuzo hiyo.

Cristiano Ronaldo, mshindi huyo mara tano wa BallonD’or na tuzo ya mfungaji wa goli bora la msimu uliopita wa klabu bingwa ulaya licha ya kutofanya vizuri na Real Madrid katika Laliga, aliisaidia kwa kiasi kikubwa kushinda taji la 13 la klabu bingwa ulaya huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake 15 likiwemo bao lake katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Juventus lililoshinda tuzo ya goli bora la msimu la klabu bingwa ulaya.

Rekodi kadhaa alizoweka msimu uliopita ikiwemo kuwa ni mchezaji wa kwanza kufunga bao katika mechi 11 mfululizo za klabu bingwa ulaya pamoja na kushinda tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya sita mfululizo na kuisaidia kushinda ubingwa mbele ya Liverpool, inamfanya kuwa ni mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo katika usiku wa leo.

Mohamed Salah, alikuwa na msimu bora sana ambao wengi hawakutarajia kutokana na alichokifanya, alifunga jumla ya mabao 44 katika mashindano yote akilingana na Cristiano Ronaldo huku akiwa nyuma ya Lionel Messi ambaye alifunga mabao 45 na kuisaidia Liverpool kucheza fainali dhidi ya Real Madrid ambayo aliumia katika mchezo huo na kushuhudia Liverpool ikipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

Pia alishinda tuzo ya (PFA) mchezaji bora wa EPL pamoja na kiatu cha dhahabu kwa mabao yake 32 katika ligi hiyo. Tuzo zingine alizoshinda ni mchezaji bora wa mwaka barani Afrika, tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika na kumfanya kuwa ni mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo kwa mara yake ya kwanza.

Luka Modric, kiungo huyo ameng’ara katika michuano ya klabu bingwa ulaya akiwa na Real Madrid na kuisaidia kushinda ubingwa, pia alionesha kiwango kikubwa katika michuano ya kombe la dunia na kuiongoza timu yake ya taifa ya Croatia kufika fainali ya michuano hiyo licha ya kupoteza kwa mabao 4-2. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika michuano hiyo ya kombe la dunia na kuandikisha historia kwa nchi yao kufika hatua hiyo kubwa katika kombe la dunia.

Wednesday, August 29, 2018

MADUKA 10 YATIWA KUFULI, UKAGUZI WA WAUZAO DAWA ZA MIFUGO MKOANI MWANZA



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Baraza la vetenari nchini limeyafunga maduka kumi ya pembejeo za mifugo jijini mwanza baada ya kubaini kuwa maduka hayo hayana leseni ya kufanya biashara ya kuuza pembejeo pamoja na kutokuwa na wataalam wa mifugo.

Mkaguzi wa baraza hilo DKT.GEORGE MTINDA amesema kuwa wamiliki wa maduka yaliyofungiwa watalazimika kulipa faini pamoja na kuajiri wataalam wa mifugo ili yaweze kuendelea na biashara ya pembejeo.

Katika msako huo, Baraza hilo limebaini maduka 10 ambayo hayana wataalam wa mifugo na leseni za kuendesha biashara ya dawa za mifugo.

MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WANATAKA KUONA NINI MOURINHO ANAWAFANYIA ZAIDI YA KUJUA HISTORIA YAKE.



GSENGOtV
Taarifa za andani ya klabu ya Manchester United zinaeleza kuwa wachezaji wa timu hiyo pamoja na wafanyakazi wanaamini meneja wao Jose Mourinho huwenda akatimuliwa kazi endapo atapoteza katika mchezo wao wa Jumapili ya terehe 01/09/ 2018 dhidi ya Burnley.

Kiongozi wa United, Ed Woodward amefanya mazungumzo na Mourinho juma hili kufuatia timu yao kupata matokeo mabaya mfululizo dhidi ya Brighton na Tottenham.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kikao hicho kinafanana na kile alichofanyiwa meneja, Louis van Gaal katika siku zake za mwisho mwaka 2016 na nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho ambaye kwa sasa kunauwezekano mkubwa wa Zinedine Zidane kurithi mikoba hiyo.

Chanzo hicho kutoka ndani ya Manchester United kimesema kuwa ”Muda si mrefu, Jose atatimuliwa wengine wakiamini ataondoka endapo atapoteza mbele ya Burnley na wengine wakiamini hatokuwepo mwanzoni mwa mwezi wa tisa ,” kimesema chanzo hicho.

Inaelezwa kuwa wachezaji nane pekee ndiyo waliyoungana meneja wao, Mourinho kutoka kwenye viunga vya Carrington kwenda kwenye hoteli yao ya the Lowry baada ya kumalizika kwa mechi yao na Spurs wakati wengine wakiamua kuondoka binafsi huku Paul Pogba akitumia gari lake.

SERIKALI YATOA KAULI KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEKUFA KWA KIPIGO.


Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amezungumzia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kibeta, mkoani Kagera Siperius Eradius akitaka vyombo vya usalama kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwalimu anayetuhumiwa.

Akizungumza leo Agosti 29 wakati wa Kongamano la Kimataifa la Hisabati linalofanyika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Profesa Ndalichako amedai kusikitishwa na tukio hilo na kwamba Serikali haitamfumbia macho yeyote atakayebainika kuhatarisha usalama wa wanafunzi shuleni, wakiwamo walimu wao.

Amesema mwalimu aliyesababisha mauaji hayo hakutumwa na mtu isipokuwa utashi wake.

Profesa amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya usalama vinapofanya kazi yake na kwamba tukio hilo lisitoe tafsiri kuwa shule  siyo mahali salama kwa watoto.

 Shule ni sehemu ambayo ni salama kwa hiyo asitokee mtu akafanya vitendo ambavyo hata wazazi wajiulize harugusu mtoto kwenda shule au asiende lakini serikali itachukua hatua kwa mtu yeyote atakayefanya shule ionekane si mahali salama‘-Waziri Ndalichako

Siperius (13) anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na mwalimu akituhumiwa kuiba pochi ya mwalimu.

TWENDE TUKA-TALII HUKU TUKIISHUHUDIA TAIFA STARS Vs THE CRAINES

Usikose kwenda kpla jmosi kushangilia Taifa Star 8/09/18 kutalii na kuona mechi baina ya Taifa Stars na Uganda 'The Craines'.

Ungana na Willy Bk Tours costa zitaanzia Muleba, Bukoba, Mtla.

Kutokea Kayanga, Misenyi Mtla ni kwa Ths 100,000/tu, Itajumuisha usafiri, malazi, tiketi ya mechi, kutalii, usiku wa kampala, shoping, kutalii Masaka na Kampala nk. Lipia kupitia 0756823250 jina William Rutta. 

Passport ni ths 20,000/= (kwa wasiokuwa nazo).

 Utalii unaanza na wewe.

WILAYA YA MANYONI MKOANI SINGIDA YATENGA ZAIDI YA EKARI 5000 KUPANDA MIKOROSHO MIPYA

  Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini  yaliyofanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho ukafanyika akielezia mikakati ya wilaya yake kupanda zaidi ya ekari 5000 za mikorosho
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana wakati wa ziara ya viongozi wa bodi kuhamasiha kilimo cha zao la Korosho kwenye maeneo mapya
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akisistiza jambo kwa viongozi wa bodi ya Korosho nchini Afisa Kilimo Frank Mfutakamba kulia na Afisa Uhusiano Bryson Mshana kushoto wakati walipofanya ziara wilaya ya Manyoni kuhamasisha kilimo cha zao hilo.
 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo ,Umwagiliaji na Ushirika  wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala
 Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa bodi ya Korosho waliotembelea wilaya hiyo kushoto  ni Afisa Uhusiano Bryson Mshana kulia ni Afisa Kilimo Frank Mfutakamba
 Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa kushoto akiagana na Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Frank Mfutakamba mara baada ya viongozi wa bodi ya korosho kumaliza mazungumzo naye
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo na viongozi wa bodi ya Korosho mara baada ya kumalizia mazungumzo nayo kushoto ni Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana na kulia ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba
 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana akitazama moja ya mikorosho mipya iliyopandwa kwenye shamba mfano ambalo walilitembelea ili kuweza kuhamaisha zao hilo liliopo Kijiji cha Masigati
NA MWANDISHI WETU,MANYONI.

WILAYA ya Manyoni mkoani Singida imetenga zaidi ya ekari 5000 kwenye Kijiji cha Masigati kwa ajili ya kupanda mikorosho mipya baada ya wananchi kuhamasisha kupanda zao hilo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya korosho nchini ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini ambao yalifanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho.

Viongozi wa bodi hiyo ambao walifika kwenye shamba la mfano lililopo katika Kijiji cha Masigati kwenye Halmashauri ya Manyoni ambalo lilianza mwaka jana ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba na Afisa Uhusiano Bryson Mshana wakiwa kwenye uhamasishaji wa kilimo hicho kwenye maeneo mapya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya hizo ekari zilizopandwa ni 1250 kwa msimu uliopita wa kilimo na msimu umekaribia mwezi Desemba mwaka huu wataanza tena kuendelea na upandaji wa mikorosho mipya.

“Pamoja na kwamba tumetenga ekari 5,000 kwa ajili ya kulima kilimo cha Korosho lakini mipango yetu ni kufikia ekari 10,000 alisema pamoja na hayo tutaendelea kufanya uhamasishaji kwa wananchi kuweza kuchangamkia fursa ya zao hili na kupanda mikorosho kwa wingi “Alisema.

Alisema wananchi wake wamehamasika baada ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa kupitia mikutano mbalimbali huku akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya kilimo hicho kutokana na kwamba maeneo yote yana uwezo kustawi zao hilo hivyo walipande kwani litawasaidia na kuwa mkombozi wa maisha yao.

“Lakini pia nisema kilimo hiki kimeweza kutoa fursa kwa watu kutoka mikoa mingine wameanza kulima korosho Manyoni hamasa bado inaendelea kwa halmshauri mbili za Manoyoni na Itigi licha kwamba hawajafanya kilimo cha pamoja lakini watu wanalima Korosho”Alisema

Alisema Halmashauri ya Manyoni wamekuwa na mpango wa kilimo cha pamoja kupitia ekari hizo elfu tano jambo ambalo limesaidia wananchi kupata ajira na hivyo kukuza uchumi wao kutokana na shughuli za upandaji zinazofanyika.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi aliishukuru bodi ya korosho kutokana na kwamba wao ndio wamekuwa chachu ya kuzalisha korosho kama zao la mkakati kwenye halamshauri yao limeanza na wao kama bodi walikuwa wa kwanza kuhamasisha wananchi.

Alisema kabla ya kuanza kilimo hicho Utaftiti ulifanyika na baada ya kugundua korosho inaweza kufanya vizuri hivyo bodi ya korosho waliomba ardhi na wazo lao kubwa lilikuwa la kwanza kupitia Halmshauri walifika Kijijini Masigati kuzungyumza na wananchi waliomba ardhi wakapewa eka 2000 wahamasisha vikundi vikaundwa wakaanza kugawa ardhi kwa vikundi.

Alisema kila kikundi kina ekari si chini ya 100 wameanza kusafisha mashamba wanalima korosho lakini wameamua mradi huo upanuliwe kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi huku akiwakaribisha watanzania wengine kuchangamkia fursa hiyo.

PEMBE ZA NDOVU ZAWANG'OA KIBARUANI POLISI WAWILI MWANZA



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Askari Polisi wawili mkoani Mwanza wamefukuzwa kazi baada ya kubainika wakijihusisha na biashara haramu ya uuzaji wa nyara za serikali aina ya meno ya tembo kinyume na maadili ya jeshi.

Kamanda Shanna amewataja askari hao kuwa ni H. 5461 PC Enock na H. 4165 PC Robert ambao walikutwa na vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 20 katika eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza.


"Kuna taarifa zilipatikana wapo watu wanaojihusisha na uuzaji wa meno ya tembo na Polisi walianza uchunguzi na kuwabaini Polisi hao waliokuwa wanashirikiana na watu wengine ambao na wao tunaendelea kuwasaka," alisema kamanda Shanna.

Kamanda Shanna amesema sheria ni msumeno na sheria ni kwa watu wote bila kujali tabaka hivyo amedai wanafanya msako kuwakamata wale wote wanaofanya kazi za magendo kwa kushirikiana na askari Polisi.

SHILOLE (SHISHI BBY) NA FUTE WAZINDUA RASMI RIWAYA YAO YA BROKEN HEART ,NDANI YA DUKA LA VITABU LA MAK BOOKS AND BRAINS MLIMANI CITY DAR.

Shilole A.K.A Shishi Baby Kulia akiwa pamoja na Jackson  Fute kuzindua rasmi riwaya waliyo andilka pamoja inayokwenda kwa jina la Broken Heart, uzinduzi huo ulifanywa ndani ya Duka la vitabu la Mak Books and Brains Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kuhusu BROKEN HEART: Hakuamini mahusiano yake na mtu aliyempenda yaishe kwa yeye kudumbukizwa kwenye dimbwi la msongo wa mawazo, aliyempenda aligeuka kuwa adui. 

'Mapenzi ni kitu ambacho kinaweza kukufanya chizi, sihitaji tena mwanaume maishani mwangu.' Alizungumza. 

Lakini maisha ni safari, na akiwa katika safari ya maisha alijikuta akizama kimapenzi kwa mwanaume mwingine, mwanaume aliyedhani ni tofauti na waliopita.
Bwana Jackson Fute (Kushoto) akiongea na waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua riwaya waliyo andika na Shilole.
Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Bongo Movie na sasa Mtunzi wa vitabu Bi. Zena Yusuf Mohamed Maarufu kwa jina la Shishi Baby, akielezea kwa ufupi namna alivyopata wazo la kuandika Riwaya ya Broken Heart kuwa inalenga historia yake ya kweli kabisa na kuongeza kuwa amefurahi kumshirikisha mwandishi chipukizi Bw. Jackson Fute na kazi imeenda vizuri. pia aliwaomba watanzania wamuunge mkono kwani kitabu kinauzwa kwa Tsh 15,000 tu na Online Ebook ni Tsh 3,000 kinapatikana kote Duniani.
Mhariri wa Riwaya ya Broken Heart Bi Zuhura Seng'enge maarufu kwa jina la The African Lioness ambaye pia ni Mshairi, Mtunzi, Mwandishi na Mfasiri akielezea namna alivyo ipokea kazi ya kuhariri Riwaya hiyo na kukili kwamba ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya kazi hiyo. "Moja ya changamoto nilizozipata wakati nahariri Riwaya hii ilikuwa ni utamu wa simulizi zilizokuwemo ndani mpaka nikachelewa kumaliza kazi hiyo kwa muda kutokana na kunogewa na visa mkasa"
alisema Zuhura.
 Waandishi wa Habari wakiendela kufanya mahojiano na Shishi Baby pamoja na Jackson Fute wakati wa uzinduzi wa Riwaya hiyo.
 Mhariri wa Riwaya hii  Bi. Zuhura Seng'enge akipokea Riwaya yake kutoka kw Shishi Bby
 Mmoja wa wadau Bw. Hassan A.K.A Double D wa Uswahilini Matola  nae akipokea Riwaya yake
 Bw. David Kisamfu  Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
 Mtaalam wa picha za mnato Bw. Zajilu Zaid nae akionesha Riwaya yake ya Broken Heart baada ya kuinunua
 Anaitwa Silver (kushoto) Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
Bw. Francis nae Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
 Ukiingia tuu katika Duka la vitabu la Makbooks Brains Mlimani City  utakutana na Riwaya ya Broken Heart
 Mmoja wa wanunuzi akiwa anasoma Dibaji
 Kulia ni mmoja wa wafanyakazi katika Duka la vitabu la Mak Books and BrainsBi. Fina akimpa mfuko wenye Riwaya ndani Shishi Baby ili amkabidhi mnunuzi.
Hili hapa ndio duka la vitabu la Mak Books and Brains lililopo Mlimani City hapa ndipo utapata Riwaya ya Broken Heart.
Picha zote na Fredy Njeje