ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 16, 2018

VIDEO NA PICHA 36 VIONGOZI MBALIMBALI NCHINI TANZANIA WAHUDHURIA MAZISHI YA MZEE JULIUS KAKONO MABULA



GSENGOtV
Hatimaye mwili wa Mzee Julius Kakono Mabula umezikwa hii leo jijini Mwanza katika makaburi ya RC Parokia ya Kirumba jijini Mwanza.

Majonzi na simanzi vimetawala tangu kanisani kwenye ibada ya kuuaga mwili wa marehemu hata makaburini wakati wa kuupumzisha mwili wa marehemu Julius Makono Mabula aliyekuwa mume wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi na hata vyama mbalimbali vya siasa wameshiriki katika hatua zote za safari hiyo ya mwisho ya mzee huyo ambaye enzi za uhai wake alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na hata katika kanisa la Roman Katoliki Mwanza.
Kwaheri....
This Photo Credit by ABC Studios Mwanza.
Picha enzi za uhai wake Marehemu Julius Mabula.
Katika kukamilisha ibada familia ya marehemu Julius Mabula ilijumuika pamoja na kufunga kwa sala iliyoongozwa na kanisa.
Jiografia ya umati uliojitokeza kanisani kushiriki ibada.
Kwaya ikihudumu katika sala ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Julius Mabula.
Ibada ikiendelea.
Nyimbo mbalimbali ziliimbwa.
Ibada ya mazishi katika viwanja vya makaburi ya Rc Kirumba Mwanza.
Ibada ya mazishi katika viwanja vya makaburi ya Rc Kirumba Mwanza.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi komred Angelina Mabula akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu mumewe Julius Mabula mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika hii leo jijini Mwanza.
  Watoto na wajukuu wa wakiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika hii leo ni katika viwanja vya makaburi ya Rc Kirumba Mwanza.
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waziri wa Nishati na madini Dkt. Medard Kalemani akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mwanasheria mkuu mpya wa serikali Dkt Adelardus Kilangi akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Peter Mavunde akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula ambaye pia alimwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Busega Raphael Chegeni, akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa na makada wa kada mbalimbali CCM wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakuu wa mikoa mbalimbali wakiongozwa na mwenyeji wao mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela (kulia mwenye shati jeupe na madoa meusi) wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakuu wa wilaya nao wamehudhuria hapa.
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Mhe. James Bwire akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mkurugenzi wa wilaya ya Ilemela Paul Wanga (kushoto) na Waheshimiwa wengine katika  zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Marry Tesha akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Kwa pamoja waheshimiwa wakiweka mashada.
Kwa pamoja viongozi wa madhehebu mbalimbali, makanisa na misikiti wakiweka mashada.
Kanisa Katoliki parokia ya Kirumba.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Juma Nature akimpa mkono wa pole mama Angelina Mabula mara baada ya kumalizika shughuli za mazishi.
Hatua za mwisho ndugu, watoto, jamaa na marafiki wa familia katika kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege akiwasha mshumaa kwenye kaburi la marehemu Mzee Julius Mabula.
Sala ya shukurani mara baada ya kukamilika kwa mazishi.

LSF YAUNGANA NA WADAU KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA


GSENGOtV
Shirika lisilo la kiserikali , Legal Service Facility (LSF) linalojishughulisha katika kusaidia upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria pamoja na kuwawezesha watanzania hususani wanawake kupata haki zao, leo wameungana na wadau mbalimbali katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika inayofanyika kila mwaka tarehe 16 mwezi Juni. 
Akizungumza kwa niaba ya LSF, Mkurugenzi wa miradi Bi Scholastica Jullu ameihasa jamii kuwalinda watoto hususani mtoto wa kike kwa kutoendeleza ndoa za utotoni kitendo kinachokatisha ndoto zao. 

MESSI AANZA KWA MKOSI KOMBE LA DUNIA 2018.



GSENGOtV

АRGЕNТINА VS IСЕLАND 1–1 - НIGНLIGНТS & GОАLS RЕSUМЕN &GОLЕS 2018 

UFARANSA YAANZA KWA NEEMA KOMBE LA DUNIA.


GSENGOtV
Ufaransa imefanikiwa kuibuka na ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Russia wa mabao 2-1 dhidi ya Australia.

Mabao ya mchezo huo yametiwa kimiani na Antoine Griezmann katika dakika ya 58 kwa njia ya mkwaju wa penati na la pili likitiwa kimiani na Paul Pogba (80').

Bao pekee la Australia liliwekwa wavuni na Mile Jedinak mnamo dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati.

Mechi hii imekuwa ya kwanza kushuhudiwa penati mbili ndani ya dakika 90 zikipigwa kwa pande zote.



Ushindi huu wa Ufaransa unawapa alama tatu muhimu kwenye kundi C ambapo baadaye Peru na Denmark watakuwa wanacheza pia kutoka kundi hilo.

HIVI HAPA VIPAUMBELE VITANO VYA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI.


Afya, Kilimo, Elimu, Maji na Viwanda vimetajwa kama vipaumbele vitano kwenye bajeti mbadala ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kutoka kwenye kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Hayo yamesemwa na Kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe ambaye amesema licha ya baadhi ya bidhaa kuendelea kubaki katika bei yake ileile lakini bado ameikosoa akisema haitekelezeki huku akisema serikali imekuwa haizingatii sheria ya fedha na kiasi kinachotengwa kimekuwa hakitoshelezi matumizi ya wizara husika.

" Unajua hivyo vipaumbele vitano ambavyo sisi tumeviainisha ndivyo ambavyo vimekuwa vikiendana na maisha halisi ya mtanzania wa kawaida na siyo miradi mikubwa ambayo haimgusi mwananchi mmoja mmoja.

" Mfano wamekuwa wakiangaika kuutaja mradi wa Stigler's Geoge ambao umegharimu bilioni 700 fedha ambazo zingeingia kwenye mahitaji ya mwananchi mmoja mmoja kama elimu, maji na kilimo yangepunguza ukwasi wa maisha na kuongeza maendeleo zaidi," amesema Mbowe.

TCRA IMEONGEZA MUDA WA USAJILI WAMILIKI WA BLOGU NA MAJUKWAA


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kufuatia kuwapo kwa sheria kwa wamiliki wa blogu na majukwaa ya mtandao bila kusahau radio na Televisheni za mtandao kutakwa kujisajili ili kutambulika kisheria.

ambapo mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuwa kwa wale wote ambao hawakuw na leseni kutoka TCRA wajisajili kabla ya tarehe 15/juni/2018 ambapo bada ya hapo sheria zingechukuliwa.

Mamlaka hiyo ya mawasiliano TCRA imeongezea muda wa kufanya usaili kutokana na maombi ya wadu waliojitokeza kuomba kuongezewa muda ili kukidhi matakwa ya kisheria.

Mamlaka hiyo imeongeza muda hadi kufikia 30/juni/2018.

WANAFUNZI 70,904 WACHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 70,904 wakiwemo wasichana 31,884 na wavulana 39,020 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu kati kwa mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo,  Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa ni kati ya wanafunzi 95, 337 walifaulu kwa kupata daraja la I-III na walikuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya ufundi.

Jafo kati ya wanafunzi waliochaguliwa wanafunzi 30,317 watajiunga tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 28,610 watajiunga na taasusi za masomo ya Sanaa na biashara. Alisema kuwa wanafunzi 885 watajiunga na vyuo vya ufundi ambavyo ni vyuo vya ufundi vya Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar-Es-Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kiukuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Waziri Jafo alisema jumla ya wanafunzi 11,977 wamechaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za ngazi za Astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada katika vyo vya elimu ya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)

Friday, June 15, 2018

BIASHARA YA KUKU MSIMU WA EID SOKO LA KIRUMBA MWANZA




GSENGOtV

Msimu huu wa Sikukuu ya Eid El Fitri mambo ya kitoweo kama Kuku, mbuzi na Ng’ombe ndiyo wakati wake wa kununuliwa kwa wingi na pia kuuzwa kwa bei ya juu ama bei kuwa ghali. Jembe Fm Leo kupitia kipindi chake cha Kazi na Ngoma imepita katika soko dogo la Kirumba lililoko wilayani Ilemela na kudhuru kiunga cha wauza kuku, bei ya kuku mmoja ni kati ya shilingi 12,000/= mpaka 25,000/=

Kuhusu mengineyo mambo yalikuwa hivi (Cheki video).

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA EID KWENYE MSIKITI WA ANWAR, MSASANI JIJINI DAR ES SALAAM.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika  swala ya Eid kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani,  jijini Dar es salaam leo Juni 15, 2018.




DK. BILAL AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUSOMA KURANI JIMBONI KIKWAJUNI

 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akizungumza wakatiwa Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwaniZanzibar.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.ndio 
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akimkabidhi zawadi,Salha   Mohamed   Khamis,   baada   ya   kuibuka     mshindi   wa   juzuu   tano   wa     Mashindano   ya   Kusoma   Kurani,yaliyofanyika   leo   katika   kiwanja   cha   Mapinduzi   kilichopo   Kikwajuni   visiwani   Zanzibar.Wakwanza   kulia   niMwakilishi   wa   Jimbo   la   Kikwajuni,Saleh   Nassoro   Jazeera     na     Mbunge   wa   Jimbo   hilo,   Mhandisi   HamadMasauni(watatu kulia)
 Mshiriki   wa   Mashindano   ya   Kusoma   Kurani,   Salha   Juma   Sadalla   akisoma   kurani   wakati   wa   mashindanoyaliyofanyika  leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar. 
 Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Abdilbaswit Hamis Hassan, akisoma kurani wakati wa mashindanoyaliyofanyika leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akisalimiana naMbunge wa  Jimbo la  Kikwajuni,  ambae pia  ni  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani ya  nchi,  Mhandisi HamadMasauni,  baada   ya   kuwasili  kiwanja   cha  Mapinduzi     ambako  alikuwa   mgeni  rasmi   kwenye     Mashindano     yaKusoma Kurani, yaliyofanyika leo visiwani Zanzibar.Wapili kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Saleh NassoroJazeera. 
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal (watano kulia mstariwapili) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na washindi wa Mashindano ya KusomaKurani   baada   ya   kuwakabidhi   zawadi.Mashindano   hayo   yamefanyika   katika   Kiwanja   cha   Mapinduzi   visiwaniZanzibar.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, akiwaaga wananchi(hawapo pichani), waliohudhuria  hafla ya  Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja chaMapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambaepia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Mwakilishi wa jimbo hilo,Saleh Nassoro Jazeera.Picha na Mpiga Picha Wetu