ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 12, 2018

HARMONIZE AHAMASISHA WAZAZI KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI YA KUTUNZA NA KUTHAMINI MAZINGIRA MWANZA

 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva anayetamba na kutikisa Afrika kwa sasa na ngoma yake 'Kwangwaru' Harmonize mapema leo ameshiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya Saint Marys iliyoko Igoma Jijini Mwanza.

Akiwa na warembo wa Miss Mwanza takribani 20 alioongozana nao, Harmonize toka WCB amewaasa watoto wadogo wanaosoma katika shule hiyo kuwasikiliza wazazi wao na waalimu akitumia kauli ya wahenga "Asiyesikia la mkuu huvunjika guu" 

"Ninapenda sana watoto kwani ninyi ndiyo furaha ya familia mmenionyesha upendo mkubwa sana kwa kuzifuatilia kazi zangu, Najua mnazipenda kwasababu zinaburudisha na si kupotosha. Natamani sana hapo baadaye nanyi mtimize ndoto zenu" Alisema Harmonize.

Kisha akaongeza "Wazazi wenu wanawapenda ndiyo maana wamewaleta hapa shuleni kupata elimu, nawasihi muwasikilize wazazi wenu pamoja na waalimu wenu kwa umakini na kuwaheshimu kwani asiyesikia la mkuu huvunjika guu, tumeelewanaaaa" Wanafunzi wakajibu kwa pamoja "ndiyooooooo"

Harmonize amewaambia watoto hao kwamba hata yeye asingefika hapo hii leo kwani licha ya kukulia mazingira magumu, kuwaheshimu wazazi wake imekuwa silaha yake kubwa.
 Harmonize amesifia sana hali ya hewa ya jiji la Mwanza akasema inapendezeshwa na watu wake kutunza mazingira.
 Moja kati ya washiriki wa Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza ambao wanakwenda kutambulishwa usikuwa 'Hit Zone' akishiriki zoezi la kupanda miti lililoongozwa na msanii Harmonize.
 "Watoto wakilelewa kwenye maadili ya upandaji miti na utunzaji mazingira watakuwa watu wema kwa taifa letu" Asema Harmonize akiwa Shule ya Saint Marry's jijini Mwanza.
 Warembo wote wamepanda miti mahala hapa.
 Rick Junior ni moja kati ya wadau WCB Mwanza naye kapanda mti shuleni hapa.
 Mtoto mtiifu kikazi zaidi.
 Pozi la watoto wetu najua kwa siku za baadaye watajivunia kitu toka eneo hili.
 Mama na wana.....
 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva anayetamba na kutikisa Afrika kwa sasa na ngoma yake 'Kwangwaru' Harmonize mapema leo ameshiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya Saint Marry's iliyoko Igoma Jijini Mwanza na hapa alikuwa akisaini kitabu cha wageni.
 Mratibu wa Shindano la Miss Mwanza 2018 Pamela akisaini kitabu cha wageni.Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mepal Management Wakala wa Miss Mwanza 2018 , yanatarajia kuzinduliwa hii leo Mei 12 kwenye viwanja hivyo vya Rock City Mall ndani ya show la kibabe la 'Hit Zone Turn Up' lililoandaliwa na kituo cha Redio Jembe Fm Mwanza.
 Picha ndani ya ofisi.
 Maelezo.
 Makaribisho...
 Karibu mgeni.
 Kamati ya Miss Mwanza ikiwaandaa vijana mabalozi wa kesho.
Watoto wakisikiliza kwa makini na utulivu wa hali ya juu.
Historia imeandikwa jijini Mwanza hii leo.

HARMONIZE: AZUNGUMZIA BIFU LAKE NA MWARABU FIGHTER.


Msanii kutoka lebo ya WCB ambae wiki chache hapo nyuma kulikuwa na skendo za kuwa na usaliti kati yake na mpenzi wake sarah, ambapo ilisemakana kuwa mpenzi wake huyo anauhusiano na Baunsa wa Diamond Platnumz, anaeitwa Mwarabu Fighter.


Akizungumza na Host wa kipindi cha 'Kikwetu' kinachoruka kila Jumamosi ndani ya Jembe Fm Mwanza anayekwenda kwa jina la Natty E swali lilikuwa hivi:-

NATTY E BRANDY - Yajayo yanashtua sana, Eh bana ee watu wameniuliza maswali mengi sana ila swali kubwa wakasema nidili na ujumbe uliouandika mwenyewe Instagram ujumbe unasema "Mara kumi ningesikia Mboso anakula mzigo ningemsubiri paleeee........Yaani ile anaingia tu nikamuulia hapo hapo. Sasa mtu kama huyu mimi naanzaje kumuuliza maana hata kucheka tu kwa msimu jamani Mungu huyu"

Kwa hiyo wewe na Mwarabu Fighter hamuongei kwa sasa?

HARMONIZE :- Mwarabu, Mwarabu brother wangu kabisa.

NATTY E BRANDY :- Kwahiyo ile ni kiki au vitu gani?

HARMONIZE :- No unajua kuna watu ambao wanapenda kuongea vitu ambavyo hawavifahamu.....
 BOFYA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Akiwa na warembo wa Miss Mwanza Harmonize hapa anajiachia jisongi 'Kwangwaru'
Warembo wa Miss Mwanza ndani ya studio za 93.7 Jembe Fm kwaajili ya mahojiano. 
Mwalimu wa warembo wa Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza ambaye pia ni mtangazaji pia Dj wa 93.7 Jembe Fm Mustapha Kinkulah amesema ingawa bado mchakato wa usajili wa warembo unaendelea lakini mpaka sasa kuna muitikio mkubwa wa warembo kujitokeza na kuomba nafasi ya kushiriki.

"Siku za usoni baada ya kuingia kambini tunategemea kufanya mchujo kisha tutapata tui la maana, kwani tumedhamiria na tumepania kwamba Miss Tanzania safari hii lazima atokee Mwanza" Alisema Kinkulah.
Ushindani wa weredi ulihusishwa kupitia maswali yenye akili ........
Mrembo alipo ambiwa kununa........
 Leo Mei 12, Harmonize anatarajiwa kufanya makamuzi ya hatari kwenye viwanja hivyo vya Rock City Mall ndani ya show la kibabe la 'Hit Zone Turn Up' lililoandaliwa na kituo cha Redio Jembe Fm Mwanza, chini ya watangazaji wake Natty E Brandy, Babajuti na Deejay Jacko. Show hilo likipewa nguvu na Jembe ni Jembe.
 'Kwangwaru'

HALINA UBISHI 'SIMBA NDIYO BINGWA 2018'


Tazama Shomari Kapombe alipoipatia Simba bao la kuongoza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ukipigwa kwenye dimba la Namfua Singida. Azam Sports 2 iko LIVE

TFF AWAONDOA WAA WAWILI KATIKA MASHINDANO.

Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro.

Waamuzi walioondolewa katika orodha hiyo ni Seleman Nonga kutoka Arusha aliyekuwa katika kituo cha Geita na Dadu Fadhil Msemo wa Kilimanjaro aliyekuwa kituo cha Singida.
Nonga ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba A7 kati ya Kumuyange FC dhidi ya Ambassador.

Msemo ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba C6 kati ya Temeke Squad dhidi ya Mtwivila City.

Waamuzi hao wawili wanatakiwa kuondoka kwenye vituo vya Geita na Singida leo Jumamosi Mei 12,2018.

TFF haitawavumilia waamuzi watakaoendelea kuchezesha chini ya kiwango katika mashindano hayo ya RCL pamoja na mashindano mengine yote kwakuwa TFF imejielekeza katika uchezeshaji wa haki katika mashindano yake yote na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kuharibu mashindano ya RCL.

Cliford Mario Ndimbo
Ofisa Habari na Mawasiliano TFF

Friday, May 11, 2018

HARMONIZE APATA MAPOKEZI MAKUBWA MWANZA.

Msanii wa Bongo flava kutoka WCB Harmonize hatimaye amewasili jijini Mwanza kwa ajili ya kukata kiu ya mashabiki wake katika show iliyopangwa ikapangika ya HIT ZONE TURN UP.

Hit Zone ni kipindi cha burudani ya mipini ya vijana wa kisasa ambacho huruka hewani kila siku za juma saa 7 kamili mchana hadi 10 jioni kinataraji kuwakusanya mashabiki wake kula burudani pamoja ambapo pia moja kati ya shughuli zitakazo nogesha usik huo ni uzinduzi wa Mashindano ya Miss Mwanza na Lake zone.

Harmonize na mkewe wamefurahishwa na mapokezi hayo na kuwaomba mashabiki  wasikose kwani wamewandalia vitu vipya.

Harmonize anayetamba na kibao cha Kwangaru aliyemshirikisha Rais wa WCB Diamond, ameambatana na mkewe Sarah, na kupokelewa na baadhi ya washiriki wa mashindano ya Miss Mwanza.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mepal Management Wakala wa Miss Mwanza 2018 , yanatarajia kuzinduliwa hiyo kesho Mei 12 kwenye viwanja hivyo vya Rock City Mall.

Kiingilio ni shilingi 10,000/= tu 











Thursday, May 10, 2018

KAMA WEWE NI MPENZI WA NGOMA KALI ZA HIP HOP 'SIKILIZA ALICHOFANYA JEMBE DJz HUYU'


Kutoka Jembe DjZ mnamo tarehe 30/March 2018 muendelezo wa makali, umefanyika na this time mkali DjMike Beatz kaachia Non Stop yake nyingine inayokwenda kwa jina Urban Swagz.

Pata fursa kuisikiliza kisha nambie mizuka yake. 

TRUMP: KUNA UWEZEKANO NIKAVUNJA AJENDA YA KUKUTANA NA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI.

Trump: Kuna uwezekano nikavunja ajenda ya kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini




CHANZO/PARStODAY
Rais Donald Trump wa Marekani sambamba na kusema kuwa, ataweka wazi siku tatu zijazo nukta atakazozijadili pamoja na Kiongozi wa Korea Kaskazini, amesema kuwa, ni suala linalowezekana kuvunja ajenda ya mkutano huo.
Trump ameyasema hayo huku Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akiwa amefanya safari mjini Pyongyang na kukutana na Kim Jong-un. Akizungumza na waandishi wa habari waliomuuliza iwapo anaweza kuvunja kikao tarajiwa na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, Trump hakukadhibisha suala hilo. Amesema kuwa, pande zote mbili yaani (Washington na Pyongyang) zinataka kufikia makubaliano.
Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini
Serikali ya Korea Kaskazini imeionya Marekani kwamba sambamba na kukaribia kikao cha viongozi wakuu wa nchi hizo, Washington inatakiwa ijiepushe na uharibifu wowote wa anga ya mazungumzo hayo tarajiwa. Taarifa iliyotolewa na chama tawala nchini Korea Kaskazini imeashiria matamshi ya kila mara ya kupenda kujitanua yanayotolewa na viongozi wa Marekani hususan yanayosisitizia kuwekewa zaidi mashinikizo serikali ya Pyongyang. Kuhusiana na suala hilo chama hicho tawala nchini Korea Kaskazini kimesema kuwa ni muhimu sana kwa Marekani kujiepusha na anga ambayo inaweza kudhoofisha kufanyika mazungumzo tarajiwa kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong-un.
Trump ni mtu asiyeaminika hata kidogo
Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa, iwapo miamala hiyo ya uhasama itaendelea dhidi ya Pyongyang, basi ni Marekani yenyewe ndiyo itakayopata hasara. Weledi wa mambo wanaamini kwamba, hatua ya siku ya Jumanne ya Trump katika kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA, imewafanya viongozi wa Korea Kaskazini kutokuwa na imani hata kidogo na Marekani kutokana na miamala yake ya kukiuka makubaliano. Trump na Kim Jong-un wanatazamiwa kukutana mwishoni mwa mwezi huu, au mwanzoni mwa mwezi Juni.

SUGU URAIANI TENA.


CHANZO/MWANANCHI
Mbeya. Saa chache baada ya kutoka jela, mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesema ni mfungwa wa kisiasa, “nilifungwa kiholela na nimetoka kiholela.”
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe leo Mei 10, 2018 walifika katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga lakini walipigwa chenga ya mwili baada ya kuelezwa na askari magereza kwamba wameshatoka, hivyo kulazimika kuwafuata nyumbani. 
Akizungumza na MCL Digital leo Sugu amesema, “Sikutaka kuhoji sababu za kutolewa, jana niliambiwa jiandae kesho (leo) tutatoka, basi nasi tukasema haina shida kwa sababu sikuwa na sababu ya kuwa ndani. Naamini sikutakiwa kuwa gerezani.”
Sugu akiwa na Masonga alifika nyumbani kwake na kumkuta mlinzi pekee kutokana na mkewe Happiness Msonge kwenda Gereza la Ruanda kuwapokea.
Dakika chache baadaye Happiness na mke wa Masonga, Grace Malya walifika nyumbani hapo na kuwalaki kwa furaha huku wakikumbatiana na kucheka.
Akizungumzia mazingira ya kuachiwa kwa wawili hao, Mbowe amesema, “inaonyesha hawakuwa na sababu ya kuwepo gerezani maana mazingira ya kutolewa kwao ni tata sana.”

JEH KWIMBA ITAFURUKUTA NA HATIMAYE KUJIKWAMUA KATIKA ELIMU?


Wanafunzi wa darasa la nne wilayani KWIMBA mkoani MWANZA hawana vitabu vya kiada vya mtaala mpya ulioboreshwa na hivyo kuathiri maandalizi ya mtihani wa upimaji wa kitaifa utakaofanyika NOVEMBA mwaka huu.

Afisa Elimu Msingi wilayani humo EMMANUEL JOHNSON amesema kuwa ukosefu wa vitabu hivyo umeathiri tendo la ujifunzaji na kuiomba serikali kuharakisha zoezi la kusambaza vitabu hivyo kabla ya Juni mwaka huu ili kuepusha madhara zaidi ya kitaaluma yanayoweza kujitokeza.

Wednesday, May 9, 2018

RC MAKONDA ATOA ANGALIZO KWA WAKANDARASI "WAPIGAJI"

 Na Zephania Mandia wa g.sengo tv.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza Barabara za chini ya kiwango na kuharibika ndani ya muda mfupi jambo linalosababisha hasara kwa serikali na usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri. 

RC Makonda ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya utiaji wa saini kwa Mikataba Nane ya mradi wa matengenezo ya Barabara, Mifereji ya Maji na Culvets inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA yenye tahamani ya zaidi ya Billion 5.8 ambapo amewataka TARURA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hizo.

Aidha RC Makonda amezitaja Barabara zitakazojengwa kupitika mradi huo kuwa ni pamoja na Tegeta Nyuki, Msasani, Magomeni Makuti,Migombani, Kimara baruti, Kibanda cha Mkaa, Sheikh Bofu, Kwa Komba, Msigani, Sea clif na Mwananyamala Kisiwani.

Hata hivyo RC Makonda ametoa wiki mbili kwa TARURA kuhakikisha wakandarasi waliojenga barabara chini ya kiwango zinajengwa upya kwa gharama ya mkandarasi ikiwemo barabara ya Mabatini ambapo barabara hizo zitakuwa na mifereji ya maji, sehemu za watembea kwa miguu na Taa za Barabarani. 

Pamoja na hayo RC Makonda amesema katika uongozi wake hawezi kufumbia macho matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi hivyo atahakikisha anasimama kidete kuhakikisha Dar es salaam inakuwa na barabara zenye ubora.

Sanajari na hayo RC Makonda ametaka uwepo wa ushirikiano wa kikazi baina ya TARURA, TANROAD, TANESCO, DAWASCO na TTCL ilikupunguza ucheleweshaji wa miradi na ujenzi usiofuata taratibu unaopelekea uharibifu wa miundombinu. 

LENGO LA RC MAKONDA NI KUHAKIKISHA PESA YA WALIPA KODI INATUMIKA KUONDOA KERO WANANCHI

MAONESHO CHUO CHA IFM TAWI LA MWANZA YAONESHA DIRA YA AJIRA KWA VIJANA.



NA ZEPHANIA MANDIA, GSENGO TV
Ni maonesho kwa njia ya ushindani ambayo yamefanyika katika himaya ya Chuo Cha Usimamizi wa Fedha Cha IFM tawi la Mwanza, yanayotumika kama sehemu ya kupima uelewa wa wanafunzi wanaotaraji kuhitimu zama za usoni ambapo hapa wanazama katika utendaji kama wako kazini wakifafanua kwa vitendo masuala wanayohusika nayo.

Kwa mujibu wa mmoja wa Waadhiri wa chuo hicho Dr Lawrence Joseph anasema kuwa Maonesho hayo pia yametumika kama sehemu ya kuwasukuma vijana kwenye ukomavu wa kujieleza hasa pale wanapoitwa kwenye usaili  wa ajira mbalimbali nchini na tukio hilo sasa linatumika kama mbinu ya kupanua wigo wa wakufunzi kuzinasa ajira. 

MAY 12 ROCK CITY MALL KINAWAKA MAZEE

Msikilize Natty E Brandy wa Show ya mchana inayogengeshwa kupitia radio Jembe Fm Mwanza akifunguka kuhusu mpango mzima wa Jembe ni jembe & WCB wanaokwenda kumdondosha Harmonize Jumamosi hii May 12/2018, ndani ya Rock City Mall Hitzone Turn up show Kwa shilingi Elfu 10,000 Tu, Miss Mwanza na Miss LakeZone Kuzinduliwa rasmi...... . @harmonize_tz hapa #JembeDjz hapa ni mwendo wa wakilipusha ma #Skilz tu #mwamwi . . Sikiliza 93.7 Jembe FM kwa maelezo zaidi