ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 28, 2018

KIBADENI ATOA DARASA KWA SIMBA NA YANGA.

Kuelekea mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga, kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni amewataka wachezaji kila mmoja kucheza kwa uwezo wake ili kuonyesha kipaji alichonacho na mwisho wa siku aisaidie timu.

“Naziomba hizi timu mbili Simba na Yanga wajue kwamba jumapili wanaenda kuonyesha vipaji vyao na walichofundishwa na makocha wao, pia wanatakiwa kutulia na sio kucheza kwa kukamiana bali soka safi kama ilivyo kwa wachezaji wa nje,” amesema Kibadeni.

Aidha Kibadeni pia amewataka viongozi wa vilabu hivyo kuweza kuwalinda wachezaji ili kutunza vipaji vyao ambavyo vitawasaidia sio kwenye soka la Simba na Yanga bali hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Mchezo ambao unaweza kuamua mbio za ubingwa utapigwa siku ya jumapili April 29 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Tayari tiketi za pambano hilo zimeshaanza kuuzwa na shirikisho la soka nchini TFF.

Simba kwasasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 59 baada ya michezo 25. Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 48 baada ya mechi 23. Baada ya pambano la jumapili Simba itabakiwa na mechi 4 huku Yanga ikibakiwa na mechi 6.

TANZIA ABBAS KANDORO KATUTOKA.

TANZIA: Mkuu wa mkoa mstaafu Mzee Abbas kandoro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar alikolazwa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopatikana msibani, Leo asubuhi saa tatu mwili umeandaliwa pale Muhimbili hospital, na ibada ya kumwombea marehemu itafanyika saa saba mchana katika msikiti wa manyema kariakoo mtaa wa mafia,na baadaye mwili utakwenda nyumbani kwake mbweni luis kwa ajili ya kuuaga mwili na saa 10.00 jioni safari ya kwenda Ihemi Iringa. 

Marehemu atazikwa siku ya jumapili saa 10.00 jioni shambani kwake Ihemi,Iringa. 

Mola aiweke ROHO ya marehemu pahala pema peponi AMIN  - #JembeHabari


Friday, April 27, 2018

HAFLA YA KUMUAGA ALIYEKUWA KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA.

Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Kamishna wa Polisi Clodwig Mtweve mara baada ya kukabidhi ofisi amefanyiwa sherehe ya kuagwa na watumishi aliofanya nao kazi kwa ukaribu kwa kipindi chote cha ajira, shughuli iliyofanyika katika bustani za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Kamishna Mtweve amekabidhi majukumu ya ofisi kwa Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella, Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza pamoja na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Hafla ya kumuaga Kamishna Mtweve imefanyika jumatano ya Aprili 25, 2018.
Rais John Pombe Magufuli alimteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2016 kuwa Katibu Tawala mkoani Mwanza ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Kabla ya Uteuzi huo Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.

RC MONGELLA AFUNGUA SEMINA YA WALIMU WA MADRASA INAYOENDESHWA NA TAASISI YA FAITH ASSOCIATION.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amefungua semina ya walimu wa madrasa inayoendeshwa na Taasisi ya FAITH ASSOCIATION kutoka Uingereza.

BREAKING NEWS: MDOGO WA JOHN HENCE AUAWA KWA KUCHOMWA KISU.

Mdogo wa Mbunge wa John Heche anayejulikana kwa jina la Suguta, ameuawa kwa kuchomwa kisu.

Kwa mujibu wa John Heche mdogo wake amechomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari waliomkamata baada ya kumkuta bar akinywa pombe, huku akiwa na pingu mkononi.

"Ni kweli kwamba mdogo wangu ameuawa na polisi, na ameuawa akiwa mikononi mwa polisi, jana usiku polisi walimkamata akiwa kwenye bar alikuwa na wenzake wanakunywa pombe, sasa wakamkamata, wameenda naye mpaka kituo cha polisi akiwa mzima wamemfunga pingu, askari mmoja akatoa kisu akamchoma eneo la mgongo kikaenda mpaka kikagusa chembe ya moyo, wamemchoma kisu akiwa wamemfunga pingu tena akiwa kituo cha polisi", amesema John Heche.


Mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika (Mortuary) ya Tarime.

BABU SEYA NA MWANAE KUANGUSHA BURUDANI YA KUFA MTU KWA WAKAZI WA MWANZA


KWA mara ya kwanza wakazi wa Mwanza na mikoa jirani wanakwenda kushuhudia burudani waliyoikosa kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki wa bendi pale ambapo wakali wa siku nyingi kwenye muziki huo Nguza Viking na mwanae Papii Kocha watakapo shuka jijini humo na kutoa burudani ya muziki live.

Papii kocha aliyetamba na kazi zake kama Salima, Fanta, Moyo, na Seya ngoma aliyoimba na baba yake Nguza Viking kwa hivi sasa anatamba na mkwaju wake mpya unaoitwa 'Waambie'.

Daaah huyu jamaa niliwahi kusema akirudi kuimba Tena Dunia itasimama.

Yasome mashairi yake hapa.

Verse 1.

Dunia inazama, naangalia, 
Sina cha kufanya,moyoni naumia.
Mawazo yangu oh, naangamia
Uko wapi Mungu wangu we,hunioni nalia

*Kumbe ulikua unanisikia , unaniangalia.....weweeee
Likapotea,tumaini langu ila imani ikaingiaa....×2

Chorus

Waambie, uliniona,nilipokuomba uliskia,na ukaitika.
Mungu wambie,uliposema uwaja, wala hukukosea njia, na ulifika.
Mungu wambieee, niwewew tuuu, niwewee tuuu, wuwuwu.
Mungu wambie eeh, niwewe tuu uliesababisha leo imefika.

Verse 2.
Wambie, kila siku ni zawadi, hakuna heshima inayozidi uhai.
Ni Nineema na Rehema, wawe ha hekima unazitimiza ahadi,
Ooh ooh wambie, hawapaswi kukata tamaa, sababu daima haupo mbali.
Ukipotea mwanga, gizani ndo nyota hunga'aa mwanga mkali.

Wambie, 
Wasiache tumaini ndo imaniiii iii
Wasiache kukuamini ndo amanii ii iii

Chorus

Waambie, uliniona,nilipokuomba uliskia,na ukaitika.
Mungu wambie,uliposema uwaja, wala hukukosea njia, na ulifika.
Mungu wambieee, niwewew tuuu, niwewee tuuu, wuwuwu.
Mungu wambie eeh, niwewe tuu uliesababisha leo imefika. ×2



Thursday, April 26, 2018

COCA-COLA NYANZA BOTTLERS YAMWAGA ZAWADI ZA PROMOSHENI YA 'MZUKA WA SOKA'

Kampuni ya Coca-Cola Nyanza Bottlers ya Mwanza imemwaga zawadi kwa washindi wa promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka inayoendelea.Wakazi 16 wa kanda ya ziwa wiki hii wameweza kukabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki 7,luninga bapa 7,na 2 fedha taslimu.
Zawadi hizo zimekabidhiwa na Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo,Samwel Makenge,ambaye alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola iliwaweze kujishindia zawadi kwa kuwa bado ziko nyingi.
Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza.
Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza
Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza.
Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza.
Baadhi ya washindi katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

HII NDIYO TAREHE 26 NA HALI YA MITAA YA JIJI LA MWANZA



GSENGOTV.
WAKATI Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa huo Mhe. John Mongella akiwakaribisha wawekezaji kuwekeza ndani ya mkoa wake huku akisisitiza kuwa ni sehemu salama ya uwekezaji, yenye tija na faida.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi kwa nyakati tofauti hii leo ameviongoza vikosi vyeke vya ulinzi na usalama kupita katika maeneo mbalimbali mkoani hapa kukagua hali ya ulinzi na usalama kufuatia habari zilizozagaa kwa kasi mitandaoni kuwa kungekuwa na maandamano kote nchini ya kuipinga Serikali iliyopo madarakani, ambapo jeshi hilo lilipiga marufuku liki bainisha kuwa halijayabariki maandamano hayo.

Gsengo Tv imepita maeneo mbalimbali muhimu (husussani yale ambayo kama likitokea la kutokea ndiyo haswaa huguswakatikati ya jiji la Mwanza kutizama shughuli mbalimbali za hapa na pale ikiwa ni pamoja na kupigia mstari hali ya usalama.

Hiki ndicho kilichojiri hadi jioni ya leo tunakwenda mitamboni.

TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 54 YA MUUNGANO NA AMANI YAKE.

Tanzania yaadhimisha miaka 54 ya muungano, wapinzani waitisha maandamano
Tanzania leo inaadhimisha miaka 54 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuunda taifa moja la Tanzania 

LIVE - SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KUTOKA UWANJA WA JAMHURI DODOMA


Ni maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania yakifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, yakipambwa na burudani za aina mbalimbali ikiwemo gwaride pamoja na halaiki. Mgeni rasmi katika sherehe hizi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Wednesday, April 25, 2018

USITHUBUTU KUKUTWA NA HII MUTU....!!


Hope you birthday is amazing as you are my best friend! I wish you love, hope and everlasting joy and happiness.
HAPPY BIRTHDAY MR. KASILE

BWENI LA WASICHANA SENGEREMA ISLAMIC LATEKETEA KWA MOTO



NA.ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV.
Bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Sengerema Islamic mkoani Mwanza limeteketea kwa moto na kusababisha wanafunzi 30 kukosa mahali pa kulala huku vifaa vyao ya shule vikitetea kwa moto vikiwemo madaftari ,vitabu,magodoro pamoja na nguo zao. 

Ni Shule ya Sekondari ya Sengerema Islamic iliyopo Wilayani Sngerema Mkoani Mwanza ambayo bweni la wasichana limeteketea kwa moto huku chanzo cha moto huo kikidaiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyotekea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani wanajisomea.

Kutokana na  wilaya ya Sengerema kutokua na gari la zima moto ,inaelezwa kuwa pindi ipatapo majanga ya moto  hutegemea huduma za zimamoto zilizopo mkoani Geita ambapo kuna umbali wa zaidi ya kilometa 60 kufika wilayani humo.

Hawa ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Sengerema Islamic ambako ndiko  bweni la wasichana limeteketea kwa moto hapa wanaeleza hasara zilizopatikana kutokana na moto huo.

Yusuph Shabani ni mkuu wa shule ya Sekondari ya  Sengerema Islamic  na Hamis Mwagao maarufu kama (Tabasamu)ndiye mkurugenzi wa shule hiyo hapa wanaelea hali ilivyo na kuiomba serikali kuwapelekea huduma ya zimamoto wilayani humo.  
Emmanuel Kipole,ni mkuu wa Wilaya ya Sengerema hapa anaeleza mipango ya serikali katika kuhakikisha kuwa wanakua na gari la zimamoto wilayani humo.

Ajali hiyo ya moto iliotokea katika shule ya sekondari ya Sengerema Islamic na kuteketeza bweni la wasichana  imesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 38.

KUTANA NA MAMA MPARA SAMAKI ANAJIITA 'SURA YA BABA SHAROBARO ALIYEPINDA'


Uvuvi ni moja ya shughuli kubwa inayofanyika katika Ziwa Victoria. Sekta hii ya uvuvi inachangia asilimia saba ya uchumi wa mkoa kwa mujibu wa tovuti ya mkoa. 

Inaelezwa kwamba shughuli za uvuvi ndizo zinazoongoza katika kuingiza fedha za kigeni katika mkoa huu na kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2011, mkoa ulikuwa na jumla ya wavuvi 52,942 huku boti na mitumbwi ikiwa 14,480.

Ili samaki aingie sokoni kwa walaji hana budi kutayarishwa, na hatua ya kwanza ya matayarisho ni kuondoshwa magamba twaita 'Kupara samaki'

Ukifika mwalo wa Kamanga uliopo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza utakuta makundi kwa makundi wanawake na wanaume vijana wakiwa nyuma ya meza zao za kupara samaki, wakiwa 'bize' na harakati za kuhakikisha kuwa wanakamilisha huduma husika.

VIELELEZO:-
Ni kielelezo tosha kwamba hii ni ajira sasa.
Nini changamoto za wadau hawa?
Wanakutana na nini?
Jeh utamtambuaje samaki aliye china?
Jeh samaki aliyevuliwa kwa sumu anajulikana?

Kutana na mwanamama huyu maarufu kwa jina la 'Sura ya Baba' 'Sharobaro aliyepinda' msikilize ujifunze kitu katika KAZI DARASA


MALARIA YAPUNGUA MPAKA ASILIMIA 7. 3 NCHINI.


Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akionyesha rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako – kwanza kulia, Balozi wa Uswizi ha Tanzania Florence Tinguell na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas. 


Na Ripota wetu Kasulu, Kigoma 

MAAMBUKIZI ya viashiria vya ugonjwa wa Malaria Nchini Tanzania yame pungua kwa Watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 na kufikia asilimia 7.3 kwa Mwaka 2017 hii ni kuzigatia harakati zinazo fanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mashirika ya Marekani (USAID) pamoja na shirika la WHO kuhakikisha wanautokomeza ugonjwa huo. 

Akizindua takwimu zilizo tolewa na Ofisi ya Takwimu ya Tanzania leo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu , alisema Siku ya leo kupitia maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa Kigoma, atazindua rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017. 

Kwa Mujibu wa Mkurugenzi mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Albina Chuwa alithibitisha Matokeo ya sasa ya utafiti huu, yanaonesha kuwa kiwango cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Tanzania kimeshuka kwa Zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3. Hii ni kwa kutumia kipimo cha haraka cha utambuzi wa vimelea (mRDT). 

Waziri Ummy alisema utafiti huo unaonesha Mikoa yenye kiwango kikubwa cha watoto wenye malaria ni, Kigoma (asilimia 24.4), Geita (asilimia 17.3), Kagera (asilimia 15.4) na Tabora (asilimia 14.8) ambapo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe na Dodoma ina kiwango kidogo cha maambukizi chini ya asilimia moja. 

"Takwimu hizi, zinaonesha kupungua kwa kiwango cha malaria kwa kiasi kikubwa, na hii ni habari njema kwetu sote na inaonesha ni jinsi gani Serikali yenu ipo tayari kutoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa malaria inadhibitiwa na hatimae tuweze kuitokomezwa kabisa Ili kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa, tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja katika kufikia malengo tuliyojiwekea ili jamii, hasa watoto chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wajawazito ambao ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa wa malaria waweze kuepukana na ugonjwa huu", alisema Waziri Mwalimu. Alisema Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, lakini bado kuna changamoto, ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya kutokomeza malaria nchini. 

Changamoto hizo ni pamoja na Wanajamii kutotumia vyandarua ipasavyo katika kujikinga na ugonjwa wa malaria, kuwepo kwa mitazamo potofu juu afua za kupambana na malaria; mfano dhana ya kuwa viuatilifu-ukoko za kunyunyizia ukutani zinaleta kunguni na viroboto na kuwa vyandarua vinapunguza nguvu za kiume ni dhana potofu ambazo hazina ukweli wowote. Vilevile, Jamii kutoshiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na kuharibu mazaliaya Mbu. 

Kwa upande wake Mkurugenzi mwakilishi wa shirika la misaada na Maendeleo la Marekani USAID Andy Karas alisema kwa zaidi ya miaka 12 USAID imekuwa ikifanya kazi pamoja na serikali kupitia Wizara ya Afya kwaajili ya Kupambana na Malaria. 

Alisema watoto wengi walio hai leo ni kwa juhudi za serikali, kwa kushirikiana na Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria kwa Muda wote wameweza kusambaza vyandarua zaidi ya milioni 10 na kununua viuwadudu zaidi ya milioni 20 na kupuliza dawa ya Mbu kwenye maeneo hatarishi vile vile wameweza kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kufanya takwimu mbalimbali juu ya kupungua kwa ugonjwa wa Malaria. 

Nae Balozi wa Usizwi Florence Tinguell aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kwa juhudi kubwa walizo zifanya katika kuhakikisha wanatokomeza Malaria ,imeweza kubuni mbinu. Kwa zaidi ya miaka 50 Ubalozi wa Uswizi umekuwa ukifadhili tafiti za malaria ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi ya Ifakara Health Institute. 

Hata hivyo mjumbe wa kamati ya bunge ya kupambana na Malaria ( TAPAMA) na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa Rose Tweve alisema wao kama wabunge wanatoa wito kwa Wananchi wote kuwa jukumu la kupambana na Malaria na mapambano dhidi ya Malaria ni la Wananchi na wasiiachie serikali peke yake na kuomba nguvu kubwa ielekezwe kwenye kinga na wahudumu wa Afya na wakina mama kufika hospitali kwa wakati ilikuweza kupatiwa kinga ya Malaria.

Kilele cha Maadhmisho ya Malaria kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni– kwanza kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Takwimu Tanzania – NBS Albina Chuwa.


Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa Serikali na viongozi wa mashirika mbali mbali ya kimataifa, wakiwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu kushoto akipokea ramani ya Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyopungua kwa malaria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Malaria Duniani Mkoani Kigoma,pichani kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Afisa Mradi JOHNS HOPKINS  VectorWorks  Jacqueline Madundo akitoa maelezo mafupi kuhusu mfumo unaosimia uwajibikaji katika maswala ya vyandarua nchini kwa Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa  kilele cha Maadhmisho ya Malaria yaliyofanyika leo katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
Kundi la muziki wa Bongo fleva la WEUSI wakiwa jukwaani kutoa Burudani na Elimu juu ya kinga ya ugonjwa wa Malaria ambayo imehadhimishwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Kundi la wananchi lililojitokeza katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ili kusikiliza ujumbe kuhusu Malaria, mgeni rasmi wa tukio hilo ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (MB).

Kikundi cha ngoma kutoka Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kikiburudisha Viongozi na wananchi waliofika katika viwanja vya Umoja ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo kwa mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25 katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.

RWANDA YAFUNGA RADIO YA KIKRISTO YA MAREKANI KWA KUCHOCHEA CHUKI.

Rwanda imeipokonya leseni kituo kimoja cha radio cha Kikristo kinachomilikiwa na Marekani, kwa kueneza chuki.
Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano Rwanda (RURA) imeifunga idhaa ya Amazing Grace Christian Radio, kwa kukiuka kanuni za matangazo.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumanne, RURA imesema imeamua kufunga radio hiyo inayomilikiwa na Marekani kwa kushindwa kufuata maadili ya umma sanjari na kukiuka thamani na tamaduni za nchi hiyo ya Kiafrika.
Miezi miwili iliyopita, Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano Rwanda ilisimamisha matangazo ya radio hiyo kwa muda wa mwezi mmoja, kwa kupeperusha vipindi vya kueneza chuki za kidini, mbali na kuwadhalilisha wanawake.
Rwanda kwa sasa inaadhimisha siku 100 za kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994, yaliyochochewa pakubwa na radio
Mamlaka hiyo imeashiria kuwa, Januari 29 mwaka huu, mtangazaji mmoja wa Amazing Grace Christian Radio inayomilikiwa na Marekani aliwadhalilisha wanawake kwa kusema kuwa ni waovu, huku akizikashifu na kuzitupia cheche za maneno makali dini nyinginezo.
Rwanda na Marekani zimekuwa katika msuguano wa chini kwa chini katika miezi ya hivi karibuni, kwani mapema mwezi huu Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kusimamisha kwa muda usiojulikana mpango wa kutozitoza ushuru nguo zinazoingia nchini humo kutoka Rwanda, uliokuwa ukitekelezwa chini ya mpango wa African Growth and Opportunity.
Hatua hii ilijiri baada ya Rwanda kuongeza ushuru wa forodha uliokuwa ukitozwa nguo kuu kuu (mitumba) zinazoingizwa nchini humo kutoka Marekani.

UZINDUZI WA ZOEZI LA KUGAWA VITABU JIJINI MWANZA.

 Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongela amezindua zoezi la ugawaji wa vitabu kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu katika shule za msingi za halmashauri ya Jiji la Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amekabidhi vitabu vya Masomo ya kuandika,kusoma,Afya na mazingira,Michezo na sanaa,maarifa ya jamii na kiingereza vilivyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI vyenye thamani ya bilioni 1.3 kwa ajili ya darasa la 1,2, na la tatu kwa ajili ya Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni idadi ya vitabu 500,446.


Lengo la Serikali ni kuhakikisha uwiano unakuwa kitabu 1kwa Mtoto 1. Mhe Mongella: Makabidhiano hayo yamefanyika s/m Buhongwa.



VIDEO:- SALAH AIONGOZA LIVERPOOL KUKANYAGA MGUU MMOJA KUTINGA FAINALI HUKU ROMA IKISUBIRI MUUJIZA MWINGINE.

Mo Salah ametengeneza moja kati ya muda muhimu wa thamani katika maisha yake ya soka na kwa klabu yake ya Liverpool kwa kuisogeza hatua kadhaa timu yake kuzifikia Fainali za michuano mikubwa Barani Ulaya.
Lakini yaweza kuwa sivyo kama inavyotabiriwa, kwani katika mchezo wa marudiano yaweza ukawa mgumu tofauti na inavyodhaniwa baada ya Roma kurejea mchezoni kwenye dakika za lala salama.
Waitaliano hao wamepata magoli ya jioni ya kustukiza kiasi cha kuweka akiba ya ndoto yao kama watatumia vyema mchezo wa marudiano nyumbani kwao.

Edwin Dzeko na Diego Peroti ndiyo waliwapa Roma Matumaini pengine ya kuweza kupindua matukeo katika mechi ya marudiano itakayofanyika jijini Roma Italia kila mmoja akisaidia kufunga bao moja na kufanya mchezo huo kumalika Kwa ushindi wa bao 5-2 walioupata Liverpool.

Edwin Dzeko ni dume la kuogopeka baada ya kuiongoza timu yake kuchomoza na ushindi kwa kuiaibisha Barsa bao 3-0 kwenye mchezo uliopita na hatimaye kufika hapa walipo sasa ndiye anayebaki kuwa tegemeo na hatma ya Roma. 
If Roma's fight-back took the gloss over what was until the last 10 minutes one of Liverpool finest-ever European nights, then it should not detract from Salah's masterpiece.
Hadi mwisho wa mchezo:-

Tuesday, April 24, 2018

WAZIRI WA AFYA AZNDUA UGAWAJI WA VYANDARUA VYENYE DAWA YA MUDA MREFU KIGOMA

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ''Vyandarua bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona''.Waziri Ummy akizungumza leo kwenye ugawaaji wa Vyandarua katika Zahanati ya Mwandiga mapema leo,mkoani Kigoma.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. Kulia ni mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas. 
Mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Asha Juma baada ya uzinduzi wa ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. 

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendeshwa na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work  chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. 



*Vyandarua Bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza Waganga Wakuu Wa Mikoa,Wa Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka Matangazo katika Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za upimaji na Matibu ya Malaria ni bure na Wananchi hawatakiwi kulipia kwakuwa kuna wafadhili wanao gharamia gharama hizo. 

Maagizo hayo aliyatoa jana Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga Wakati akizindua ugawaji wa Vyandarua endelevu vyenye dawa ya Muda mrefu ,kwa Wakina Mama wajawazito na Watoto wenye umri wa Mwaka Moja wa ushirikiano wa Serikili ya Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria na Shirika la misaada la marekani (USAID) ambapo alipokea Malalamiko kutoka kwa Wananchi wakidai kutozwa fedha kwaajili ya Matibabu na Wakati serikali imeagiza Zoezi hilo ni bure. 

Waziri Mwalimu alisema Ugawaji endelevu wa Vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la JohnsHopkins Center for Communication na Vectorworks kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID) kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti malaria Na kuratibiwa na Serikali kupitia Mradi wa Kupambana na Malaria NMCP kwa hiyo vyandarua hivyo ni bure na Wananchi wanatakaiwa wasilipie. 

Aidha alisema ofisi ya takwimu (NBS) katika kaya mwaka 2017 zilionyesha kupungua kwa kiwango cha Maambukizi ya Malaria hadi chini ya asilimia 10% kutokana na Mikakati iliyowekwa na Wizara kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa Malaria. 

Alisema mikakati ya Serikali ni kuongeza kasi ya upimaji wa Malaria kwa kutumia kipimo cha (mRDT) Hadubini na Kutumia dawa za mseto pindi wanapothibitika kuwa na Vimelea vya malaria , kuwapatia Wajawazito Vyandarua vyenye viuatilifu ili kujikinga kuumwa na Mbu pia kuwapatia dawa za Sp kwa kipindi maalumu wakati wa ujauzito ilikuwakinga na madhara yatokanayo na Malaria. 

"Niendelee Kusisitiza dawa za malaria na Matibabu ni bure Wananchi hawatakii kulipia, wafadhiri wetu wanajitoa sana kuhakikisha Suala la Malaria liishe , Waganga wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na namba za simu kwenye vituo vya Afya iliwananchi watakao lipishwa watoe Malalamiko yao ilikuweza kuondokana na changamoto ya Ugonjwa wa Malaria", alisema Mwalimu. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini , Elisha Robarti alisema zahanati hiyo inakabiliwa na upungufu wa Watumishi wahitaji ni watumishi 15 na waliopo ni watumishi saba hali inayopelekea Watumishi kulemewa. 

Wakitoa Malalamiko yao Wananchi waliofika kupata huduma Katika Zahanati hiyo mbele ya Mh Waziri, Lydia Leonard alisema Wamekuwa wakitozwa shilingi 2500/= kwaajili ya Kipimo cha Malaria na kulipa dawa wanapofika kwaajili ya Matibabu . 

Alisema pamoja na kuwa na Kadi ya bima ya Afya lakini bado wanaendelea kutozwa fedha na kumuomba Waziri kusimamia suala hilo iliwaweze kupata Matibabu bure kama serikali inavyo elekeza. 
  

Hata hivyo Wananchi hao Shukuru Issa aliomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya Kata ya Mwandiga pamoja na kuboreshewa huduma Za Maji kwani maji wanayo yatumia sio salama na Wanalazimika kutumia Kilomita 13 kufuata huduma na Waziri alitoa maelekezo kwa halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini kuanza ujenzi wa kituo hicho kwakuwa kata hiyo inawatu wengi na inahitajika kupata kituo cha Afya.

MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

 Msanii Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini (kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
 Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari.

Msanii nguli  wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018  uitwao Colours.

Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki  Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na  kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla.

“Kwangu hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha  ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond

Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna imani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano haya”alisisitiza.

Prodyuza nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa. “Ninayo furaha ya kufanya kazi  na Diamond kwa mara nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima kubwa tuliyopewa”

BWENI LA WASICHANA SHULE YA SENGEREMA ISLAMICK LAUNGUA MOTO KWA SHOTI YA UMEME.




Bweni la wasichana Shule ya Sengerema Islamick laungua moto kutokana shoti ya umeme.

Monday, April 23, 2018

KAMATI YA AMANI MKOA WA MWANZA YAJA NA MSISITIZO HUU KUHUSU MAANDAMANO.


Kamati ya amani mkoa wa Mwanza, mapema hii leo imeketi na haya ndiyo yaliyochomoza kwenye majumuisho na hatimaye hitimisho.

NYUMBA ZAIDI YA 40 ZAHARIBIWA NA MVUA KUBWA KILIMANJARO

Nyumba 40 zimeharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha katika Kijiji cha Kileo Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro , nyumba kumi zimeanguka na zingine 30 kukatika kwa nyufa huku baadhi ya nyumba zikiwa zimengirwa na maji katika kijiji hicho.

Baadhi ya wananchi walioathiriwa na tukio hilo wamesema, tetemeko, radi na mvua hiyo ilianza saa nane za usiku wa kuamkia jana lakini kwa bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa baada ya kuwahi kujiokoa.

kufuatia hali hiyo ‘waathirika hao wakiwemo wanawake  Bi Kaweresia Akilimali  na Bi. Mwajuma Amir  wameiomba serikali wilayani mwanga kuwapatia msaada wa haraka wa kurejesha nyumba zao katika hali ya kawaida kutokana na uwezo mdogo walionao wa kipato.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Kazeni Mcharo amesema kaya za nyumba hizo  awali zilihifadhiwa kwenye shule za sekondari za msingi za kijiji hicho lakini sasa wamechukuliwa na ndugu na jamaa kwa muda...insert ya bw kazeni mcharo mwenyekiti wa kijiji cha kileo.

BAADA YA MAANDAMANO MAKUBWA KUFANYIKA WAZIRI MKUU AACHIA NGAZI.


Waziri Mkuu wa Armenia, Serzh Sargsyan amejiuzulu rasmi leo April 23, 2018 baada ya siku kadhaa za maandamano makubwa ya kitaifa dhidi yake.

Wafuasi wa upinzani wanamtuhumu Sargsyan kwa kung’ang’ania madaraka mara tu baada ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu Jumanne ya wiki iliyopita, baada ya kumaliza mihula miwili ya miaka 1o kama Rais

Tangazo hilo limekuja baada ya kiongozi wa upinzani Nikol Pashinyan kufunguliwa kutoka kizuizini. Pashinyan alikamatwa siku ya Jumapili baada ya mazungumzo ya televisheni na Mr Sargsyan kutofikia muafaka.