ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 23, 2018

BREAKING: RAIS MAGUFULI AVUNJA BODI YA TEMESA

Kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere Septemba 20, mwaka huu katika Ziwa Victoria wilayani Ukerewe, Mwanza, Rais Dk John Magufuli ameivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo inasema kuwa, Bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Mstaafu, Mhandisi Mabula Mashauri imevunjwa kuanzia leo wakati kamati ya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.