ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 16, 2018

UTPC WALAANI VIPIGO VYA POLISI KWA WAANDISHI WA HABARI.



GSENGOtV
Umoja wa klabu ya waandishi wa habari  nchini Tanzania (UTPC ) umelaani hatua ya jeshi la polisi kuwakamata na kuwapiga waandishi wa habari wakiwa katika hatua ya kutekeleza majukumu yao ya kazi.


Wiki za hivi karibuni kumeshuhudiwa waandishi wa habari wawili katika mikoa ya Mara na Dar es Salaam wakijikuta katika kadhia ya jeshi la polisi wakati wakitimiza majukumu yao ya uandishi. 
Mkurugenzi mtendaji wa UTPC Karsin Abubakari ameeleza hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana mara baada ya waandishi wawili Sitta Tuma wa gazeti la Tanzania daima na Silas Mbise wa Wapo Radio kukamatwa na kupigwa na jeshi la polisi wakati wakitekeleza majukumu yao ya kazi
Ameongeza kwa kusema kuwa mara baada ya matukio ya kukamatwa kwa waandishi wa habari Tanzania, chama hicho kiliamua kuliandikia barua  jeshi la polisi ikiwemo mkuu wa jeshi hilo Inspekta Jenerali Simon Sirro lakini hawajawai kujibiwa jambo linalozua sintofahamu kwa wandishi wa habari nchini humo.
Kwa upande wake  Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania daima, Sitta Tuma ambaye agosti 8 alishikiliwa na jeshi la polisi mkoani mara na kufunguliwa mashita kwa madai kuwa amefanya mkusanyiko usiokuwa na uhalali wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi amesema  wakati umefika kwa jeshi la polisi kujitathimini na kufuata sheria na taratibu za nchi .
Katika hatua nyingine Sitta amemuomba mkuu wa jeshi la polisi nchini humo na Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola wajitafakari na kuangalia namna za kulibadilisha jeshi hilo hili kuleta mabadiliko ya kiutendaji kwa askari wa jeshi la polisi nchini Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.