ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 21, 2018

RC MONGELA AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA WATENDAJI IDARA ZA AFYA KUJA NA MPANGO KAZI WA KUTEKELEZA KAMPENI YA UHAMASISHAJI UPIMAJI AFYA ILI KUBAINI MAAMBUKIZI VVU.



GSENGOtV/-/MWANZA.
Mwezi mmoja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya “Furaha yangu, Pima, Jitambue, Ishi’ jijini Dodoma kwa ngazi ya kitaifa sasa kampeni hiyo inazinduliwa hapa ikiwa ni Julai 21 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kwa ngazi ya mkoa.
Zaidi ya matarajio, viongozi na wananchi wake kwa waume hata watoto wamejitokeza kwa wingi ili kupima na kutambua afya zao.
Mabanda ya kupima maradhi mbalimbali yamesimikwa katika viwanja hivi ambapo ni fursa sasa kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella kuyatembelea mabanda hayo kujionea shughuli za afya na elimu zinazofanyika hata ikibidi naye kupima afya.
Hizi ni Dawa mpya zenye uwezo wa kufubaza na kukinga maambukizi dhidi ya VVU kwa asilimia 99 zilizoanza kutumika katika baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika, na sasa zimekuja ukanda huu wa Afrika Mashariki ndani ya Tanzania. Badala ya kumeza vidonge vingi sasa muathirika atapaswa kumeza tembe moja tu kujikinga na maambukizi.
Naam mara baada ya kupata elimu ya kutosha Mhe. Mongella hakusita kupima afya ambapo majibu yalitoka papo hapo.
 Akizungumza  wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Mwanza Dk Pius Masele amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi yameongezeka na kufikia asilimia 7.2 kutoka asilimia 4.2, mwaka 2011
 Kwa mujibu Dk Masele amesema ongezeko hilo linaufanya mkoa huo kuwa wanne ukitanguliwa na Njombe,Iringa na Mbeya.
Dk Masele ameeleza mikakati ya kupunguza maambukizi hayo ni  kuzifikia 90 tatu, ifikapo kwama 2030.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, amewataka watendaji  wa idara za afya katika wilaya zote za mkoa huo kuhakikisha wanaandaa mpango kazi utakaoainisha jinsi watakavyo tekeleza kampeni hiyo ili iwe na tija.

Kampeni ya furaha yangu inafadhiliwa na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) Tanzania kupitia mradi wake wa FHI360- Tulonge Afya wa miaka mitano,  Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS)  na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia kipengele cha kusaidia wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 45 kwa kipindi cha miezi sita .








Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.