ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 31, 2018

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI MKUTANO WA MBUNGE JIMBO LA ILEMELA

 Picha za matukio ya mkutano wa mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula, na wananchi uliofanyika mwishoni mwa wiki katika kata ya Shibula, lengo kuu likiwa ni kusikikiza kero na changamoto zinazowakabili wananchi wake na kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.






Aidha katika hatua nyingine Dkt.Angeline Mabula ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John Wanga kwa kushirikiana na madiwani wa Kata ya Nyamhongolo na Buswelu kuhakikisha bonde la Nyamadoke haliharibiwi kutokana na shughuli za kibinadamu.
Dkt Mabula alitoa rai hiyo jana alipofanya alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa zahanati ya Nyamadoke sambamba na kuzungumza na wananchi ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku tano katika jimbo lake.
“Mkurugenzi kwa kushirikiana na madiwani hususani Kata za Nyamhongolo na Buswelu msimamie vyema bonde hili ikiwemo kuzuia ujenzi kwani ni kinyume cha sheria ya ardhi na ndio maana kwenye upimaji shirikishi eneo hilo halijahusishwa na watu wasipoteze fedha zao katika kujenga eneo hilo kwani watakuja kuondolewa”. Alisema Dkt. Mabula.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyamhongolo Victor Leonard alisema mradi wa ujenzi wa zahanati ya Nyamadoke ulianza  Agosti 2013 hadi  Januari 2014  kwa nguvu za wananchi na fedha kutoka Serikali Kuu ukigharimu shilingi milioni 17.5.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.