ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 2, 2018

MBUNGE MAJI MAREFU AFARIKI DUNIA.


Dar es Salaam. 
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM),  Steven Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu amefariki dunia leo usiku Jumatatu Julai 2,  2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Taarifa ya kifo cha mbunge huyo imethibitishwa na ofisa uhusiano wa Muhimbili,  Aminiel Eligaeshi.


Juni 20,  2018 Majimarefu alihamishiwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda MNH kwa matibabu. Hata hivyo kilichokuwa kikimsumbua mbunge huyo hakikuwekwa wazi.


Juni 6,  2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe,  Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu MNH

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.