ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 3, 2018

MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) YATOA MSAADA KWA WAZEE WA KITUO CHA KUHUDUMIA WAZEE CHA FUNGAFUNGA, MOROGORO


 Bibi. Yolanda Mkapa (aliyesimama) akitoa utambulisho na kuwakaribisha wawakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ambao walifika katika Kituo cha kuhudumia wazee cha Fungafunga Mkoani Morogoro.
 Bibi Sarah Kibonde Msika (aliyesimama) akitoa maelezo kuhusu msaada ambao SSRA imetoa kwa wazee wa Kituo cha Fungafunga. Waliokaa kutoka kushoto ni Mohammed Ramadhani (Dereva, SSRA) Agnes Lubuva, Afisa Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA na Rashid Omary (kulia) Afisa Mfawidi Msaidizi, Kituo cha Kuhudumia wazee cha Fungafunga.
 Bibi. Sarah Kibonde Msika akimkabidhi Msimamizi wa Kituo cha Kuhudumia wazee Fungafunga Bibi. Yolanda Mkapa, msaada wa vitu mbalimbali kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa SSRA.
 Mzee Joseph Kaniki, Mwenyekiti wa wazee Kituo cha Fungafunga akitoa shukrani kwa niaba ya wazee wenzake baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Wazee wa Kituo cha Fungafunga wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.