ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 5, 2018

KESI YS RUGEMALIRA NA SETH YAAHIRISHWA TENA LEO..


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa IPTL, Harbinder Seth na mwenzake hadi July 19,2018 kwa sababu upelelezi haujakamilika.

Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kwamba shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Hajra Mungulla aliuomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi,
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi July 19,2018.


Mbali na Seth mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara James Rugemalira ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 300.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.