ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 3, 2018

KANGI LUGOLA AWASILI WIZARANI AFANYA KIKAO NA WATENDAJI WAKUU

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola, akiongozana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), baada ya kupokelewa   leo ofisi ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Waziri wa   Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na viongozi wengine wa
wizara hiyo akiwepo Naibu Waziri, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (wakwanza kulia). Wakwanza   kushoto  ni   aliyekuwa   Naibu   Katibu  Mkuu   wa   wizara  hiyo,Balozi   Hassan Simba Yahaya.Kikao hicho kimefanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa kikao cha viongozi wakuu wa wizara hiyo, Waziri Kangi Lugola (watatu kulia), Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (wakwanza kulia), aliyekuwa   Naibu   Katibu   Mkuu   wa   wizara   hiyo,Balozi   Hassan   Simba   Yahaya (wapili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vyama vya Kijamii, Marlin Komba (wakwanza kushoto). Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam.  
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Simon Sirro, baada ya kufika Ofisi ndogo ya wizara jijini, Dar es Salaam, leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi baada ya kufika Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam, leo. 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.