ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 21, 2018

UKIONA MTU ANAKUJA KWENU BILA UTAMBULISHO PIGA BAKORA

GSENGOtV
NJOMBE

Licha ya kuwepo kwa taarifa za waganga wa tiba asili na tiba mbadala kutumia utaalamu walio nao kuwatapeli wagonjwa pindi wanapo hitaji huduma zao,hivi sasa hali imekuwa tofauti ambapo kumelipotiwa kuwepo kwa matapeli wanao tumia mgongo wa serikali kuwatapeli waganga wa tiba asili mkoani Njombe.

Kutokana na wimbi hilo la matapeli wanaodai kutoka serikalini kumemsukuma mratibu wa waganga wa tiba asilia na tiba mbadala kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa idara ya afya MATHIAS GAMBISHI, kuwaagiza waganga mkoani Njombe kuwaadhibu kwa viboko huku wakiwapeleka polisi mtu yeyote atakayebainika ni tapeli huku akijinadi kutoka serikalini.

Tarifa kutoka Njombe inasomwa na AMIRI KILAGALILA

Gambishi ametoa agizo hilo alipokuwa akisimamia uchaguzi wa viongozi wa waganga wa tiba mbadala na tiba asilia waliopo katika chama cha TAMETO na kuwaonya waganga kutokubaliana na faini ambazo zimekuwa zikitozwa na baadhi ya matapeli bila wao kuhoji na kupata taarifa zao kamili kwa kuwa serikali inapotuma maafisa hutumia utaratibu maalumu ikiwemo uthibitisho wa barua wenye nembo ya taifa.

insert......mratibu wa waganga

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RENATHA MZINGA askari SSP A.M.HAULE amesema kumekuwepo na matukio ya waganga kutapeliwa fedha hadi kiasi cha milioni mbili hali ambayo inaweza kujenga uhasama ndani ya jamii.

Aidha kamanda Haule ametoa wito kwa waganga kuacha kukaa na nyara za serikali ikiwemo pembe za wanyama ndani ya nyumba zao kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria hivyo endapo nyara hizo zimekuwa zikitumiwa katika shughuli zao ni vema kupata kibali kutoka kwa maafisa mali asili ili kuepukana na adhabu pindi watakapobainika.

insert.........kamanda haule

Nao baadhi ya waganga akiwemo ALLY MUHAGAMA maarufu kwa jina la dk.sagasaga na Saidi mlwale ambaye ni makamu mwenyekiti wa TAMETO mkoa wa Njombe wameiomba serikali kutoa vyeti vya uponyanyi kwa baadhi ya wahubiri ambao wamekuwa wakijinasibu wanaponya huku baadhi yao wamekuwa wakiipotosha jamii.

insert........waganga akiwemo dk saga saga

Aidha kwa upande wake RAISI wa chama cha waganga wa tiba asili na tiba mbadala TAMETO nchini Tanzania SHALIF WIKETYE amewagiza waganga waliopo katika chama hicho kujisajili katika ofisi ya mratibu wa waganga mikoani mwao ili kuepukana na utapeli pamoja kukamtawa kwa makosa kutoa huduma zao bila vibali kutoka serikalini. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.