ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 22, 2018

WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA WANOLEWA JINSI YA KUANDIKA HABARI ZA AFYA.



GSENGOtV

Meneja wa Kanda ya Magharibi Mradi wa TULONGE AFYA unaofadhiliwa na USAID Mr. Sihiana Mkanda amesema kuwa mradi huo umekuja ukiwa na lengo la kubadilisha mtazamo na wa tamaduni hasi zilizozoeleka kwaajili ya matokeo chanya kwa jamii.

Katika semina iliyofanyika juni  21, 2018 katika ukumbi wa JB Belmonte Hotel jijini Mwanza iliyoandaliwa na Shirika la Internews kwa kushirikiana na Shirika la USAIB Tulonge Afya na Fhi360, na kuwakusanyisha wanahabari wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga, akitoa mada inayohusu mchango wa vyombo vya habari katika kuhamasisha matumizi rafiki katika lugha wakati wa uzalishaji wa habari za afya, Mkanda amesema kuwa Lugha ina nguvu ya kumweka mwathirika ndani ya jamii kujisikia mwenye furaha na hata kuondoa hofu ya kujiainisha.

Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine, watu wanaohusishwa na VVU wanatazamwa vibaya na kufanyiwavitendo viovu vinavyochangia kudhoofisha afya na uwezo wao wa kuishi maisha yenye tija, hali ambayo husababisha kile kinachoitwa unyanyapaa na ubaguzi. Unyanyapaa unahusu imani na mtazamo ambao kwa kiwango kikubwa hudhalilisha utu wa mtu au kikundi cha watu kutokana tu na maumbile yasiyokuwa ya kawaida au kuhusiana na VVU na UKIMWI. Hali hii huweza kusababisha vitendo vyenye kuumiza kama vile ubaguzi dhidi ya mtu huyo au kikundi hicho.
Watu walioathiriwa na unyanyapaa na ubaguzi huweza kupoteza ajira, riziki, mali na marafiki. Wengi wa watu hawa wameacha kutafuta au kuhudhuria huduma za afya kwa sababu tu ya kuhofia kunyanyapaliwa au kubaguliwa. Kwa mtazamo huu, unyanyapaa na ubaguzi vimekuwa ni miongoni mwa vichocheo vya maambukizo ya janga la VVU na UKIMWI kwa kusababisha hofu na usiri miongoni mwa watu juu ya kupima VVU na kuweka wazi hali yao ya afya.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Interviews, Wenceslaus Mushi akielezea kuhusu mradi wa Boresha Habari, namna ulivyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari jinsi ya kuandika habari za afya kwa usahihi.
Waandishi wa habari katika umakini humu wakiandika vipengele muhimu kwaajili ya kutengeneza wazo kuu.
Meneja wa Kanda ya Magharibi Mradi wa TULONGE AFYA unaofadhiliwa na USAID Mr. Sihiana Mkanda akiifafanua Kampeni ya PIMA NA TIBU 'Test and Treat all Campaign'
"Ukiwa unaandika habari, jiulize, Jeh habari ninayoiandika inaigusa jamii kwa kiasi gani, hata hiyojamii kutamani kuchangia mawazo?" Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Interviews, Wenceslaus Mushi 
"Dhana potofu zinaweza kuifanya jamii kufanya vitendo vya kunyanyapaa wengine. Watu wamedhani kimakosa kwamba VVU vyaweza kuambukizwa katika majumuiko ya kawaida na hivyo kujihalalishia vitendo vya kuwanyanyapaa wale wanaoishi na VVU kama vile kuwanyima pango, ajira n.k. Mara nyingi watu wamehusisha VVU na tabia mbaya ya uasherati hivyo kulifanya suala hilo kama jambo la aibu, shutuma na hukumu." Alisema Wenceslaus Mushi, kisha akaongeza.....

"Kwa bahati mbaya, mitazamo hii imejikita kwenye mila na desturi za jamii na kuifanya iwe vigumu kushughulikiwa"
Kwa umakini na tafakuri ndani ya semina.
Uchangiaji kutoka kwa mwanahabari ambaye pia ni Mwenyekiti wa OJADACT Mr. Soko.
Waandishi wa habari katika umakini humu wakiandika vipengele muhimu kwaajili ya kutengeneza wazo kuu.
Usikivu zaidi.
"Kupata majibu ni vyema kuliko kuishi gizani"
"Kwanini watu ni wepesi kupima lakini wazito kurudi kupata majibu?"

"Hata hivyo nimejifunza jambo kupitia ninyi waandishi wa habari, kuwa bado kuna changamoto katika jamii kuhusu uelewa na kutofautisha majibu ya NEGATIVE na POSITIVE"  Yaani ipi ni ipi na nini ni nini......! 

TAFAKARI JUU YA UELEWA WAKO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.