Aliyewahi kuwa kiungo wa Manchester City, Yaya Toure, amemchana kocha Pep Guardiola akisema ana ubaguzi kwa baadhi ya wachezaji haswa wa Afrika.
Toure ambaye ameondoka Manchester City mwezi Mei 2018 ikiwa ni baada ya kukaa kwa muda wa miaka minane ndani ya timu hiyo, amefunguka na kueleza hayo kufuatia kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na Guardiola.
Nyota huyo kutoka Ivory Coast, amefunguka na kueleza mengi huku akisema Guardiola atakuwa ana tatizo na wachezaji wa kiafrika kutokana na vitendo vya ubaguzi ambavyo amekuwa akivionyesha kwao.
Aidha, mchezaji huyo ameeleza si mara ya kwanza kuyasema hayo bali hata wakati akiwa Barcelona matukio kama hayo ya kutengwa na kocha huyo yalikuwa yakifanyika kwake huku akisema inawezekana alikuwa akimuonea wivu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.