ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 12, 2018

SHUHUDIA PALE RAIS MAGUFULI ALIPOKOPA LAKI ILI KUMPA MWANANCHI MTAJI


Rais Magufuli Asimama Barabarani Kuongea na Wananchi. RAIS John Magufuli ametoa pesa taslim kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mifuko 625 ya sementi itakayosaidi kwenye ujenzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA unaoendelea kujengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Rais ametoa mchango huo leo Juni 12, 2018 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti huo unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco. Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini Tanzania utabeba zaidi ya watu 8,000 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili au mei mwakani. “Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote,” amesema Rais Magufuli

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.