ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 27, 2018

SERIKALI YA TANZANIA YAPEWA SIRI KUBORESHA USAFIRI MIJI MIKUBWA.


CHANZO/Hellen Nachilongo, MWANANCHI

Dar es Salaam. Serikali imetakiwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuimarisha usafiri katika majiji makubwa.
Hayo yameelezwa leo   Juni 27 na Mkuu wa Sera wa kampuni ya usafiri ya Uber, upande wa Afrika Kusini, Yolisa Mashilwane.
Mashilwane amesema hayo wakati wa mkutano maalum wa kuboresha usafiri katika majiji.
Mkutano huo wa siku tatu, umewaleta pamoja wadau wa usafiri ambao walijadiliana namna ya kuifanya miji inayoendelea kukua kwa haraka.
Mashilwane amesema kama nchi zinazoendelea zitatua tatizo la usafiri katika miji mikubwa, basi na serikali itatakiwa kushirikiana  na sekta binafsi katika hilo.
“Miradi kama wa BRT(mabasi yaendayo haraka) ni vigumu kutekelezeka bila ushirikiano wa wadau. Kuna masuala muhimu yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kutekeleza mradi huu,” amesema
Hata hivyo amesema katika muongo mmoja uliopita, serikali imeunda sera na sheria mbalimbali ambazo zimesaidia katika sekta ya usafirishaji.
Ofisa wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini(Tarura), Mhandisi Benjamin Maziku alisema nchi nyingi zimejaribu kufuata mfumo wa ushirikiano wa sekta binafsi na za umma ili kuendeleza miradi ya barabara na uwekezaji mwingine muhimu.
“Kwa bahati mbaya, wananchi hawana uelewa wa baadhi ya miradi,”amesema

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.