ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 25, 2018

VIDEO:- SERIKALI YASHINDA KESI YA MITANDAO MWANZA



NA ZEPHANIA MANDIA  G.SENGOtV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemhukumu  mshtakiwa  Daudi Magesa ambaye ni fundi simu kifungo cha mwaka mmoja  nje  bila  kutenda kosa lolote pamoja na kutaifisha na kuharibu  vifaa alivyokuwa akivitumia baada ya kumkuta na hatia ya kutenda kosa la kughushi  namba tambulishi za simu (IMEI)  kinyume na kifungu namba 154 na 135/158 ya sheria ya mtandao na mawasiliano ya posta namba tatu ya mwaka  2010.
Akitoa hukumu hiyo hii leo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo,  Bahati Chitepo, amesema mahakama  imemkuta na   hatia ya makosa yote,  mshtakiwa mwenyewe kakiri kutenda kosa hilo  na vielelezo vyote vilivyowasilishwa  vinathibitisha kutenda kosa hilo.
Johaness Kalungura, Kaimu Naibu Mkurugenzi  wa Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania TCRA , amesema Watu hawa ni hatari wanatumia software na kubadilisha IMEI mtu ambaye ni mhalifu anaendelea kutenda uhalifu na asiyemhalifu simu yake inabadilishwa, wakati vyombo vya dola vinamtafuta mhalifu  vinashindwa kuwatambua  na kusababisha kukamatwa  kwa mtu asiyehusika na mhalifu anaachwa,” alisema  Kalungura.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.