ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 19, 2018

SENEGAL YAONDOA MKONO SHAVUNI MWA AFRIKA

Timu ya taifa ya Senegal (Simba wa Teranga) wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Poland, na kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kushinda mechi ya kwanza katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Katika ushindi huo Kocha wa Senegal Alilou Cisse ameweka historia kwani wakati timu hiyo inaifunga Ufaransa kwenye Finali za mwaka 2002 ndiye alikuwa nahodha.

Katika fainali hizo zilizopigwa nchini Korea ya Kusini na Japan, Ufaransa ndio walikuwa mabingwa watetezi baada ya kutwaa Kombe hilo mwaka 1998 kwa kuwafunga Brazil mabao 3-0.

Bao la kujifunga la mlinzi wa Poland na klabu ya S.P.A.L Thiago Cionek dakika ya 37, liliipa nguvu Senegal na kucheza kwa kujiamini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. Kipindi cha pili M'Baye Niang aliongeza bao la pili dakika ya 60, kabla ya Poland kufunga bao moja dakika ya 86 kupitia kwa Grzegorz Krychowiak.

Senegal sasa inashika nafasi ya pili kwenye Kundi H nyuma ya Japan zote zikiwa na alama 3. Poland na Colombia zinabanana mwisho baada ya wote kupoteza mechi zao za leo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.