ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 24, 2018

RC MONGELLA AWATAKA WAMACHINGA KUONDOSHA BIDHAA ZAO NDANI YA HIFADHI YA BARABARA KUPISHA UKARABATI WA BARABARA YA PAMBA


NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka wafanyabiashara wadogo al-maarufu kama Wamachinga kuwa wastaarabu na kupisha wenyewe bila nguvu, maeneo ya hifadhi ya barabara ya Pamba ili kupisha ujenzi unaoendelea hivi sasa.

Hayo yamejiri mapema hii leo Jumapili tarehe 24 Juni 2018 ambapo Mongella amefanya ziara ya kukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na kujionea jinsi wafanyabiashara hao wanavyo kwamisha shughuli za ujenzi kwa kutandaza bidhaa zao hadi ndani ya hifadhi ya barabara kiasi cha kusababisha wajenzi wa barabara hizo kuwa na kazi ya ziada kutekeleza wajibu majukumu yao.

 Kipande kinachofanyiwa Ukarabati nao unaoelekea mwisho kukamilika ni kile cha kuanzia eneo la Sahara Conner hadi eneo la Jengo la Kishimba sanjari na kipande kilichopo katika kona inayotoka Sahara kwenda Buhongwa. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa na Kamati ya ulinzi na Usalama mkoa, leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa barabara ya Pamba, kujionea hatua zilizofikiwa ikiwa ni katika hatua za mwisho.
Barabara ya Pamba ni  moja ya barabara muhimu ndani ya jiji la Mwanza ambayo kwa sasa imefungwa kupisha ukarabati kwani ni kipindi kirefu imekuwa ikipitika kwa tabu kutokana na kuharibika vibaya na hivyo kusababisha adha kubwa kwa watumiaji wakiwemo madereva wa magari, pikipiki na hata watembea kwa miguu.
Kuharibika mara kwa mara kwa barabara hiyo ya Pamba  inayounganisha barabara za Kenyata na Nyerere, kuliwalazimu wananchi kupaza sauti zao za malalamiko, hatimaye Wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA mkoa wa Mwanza wakasikia kilio hicho na kuchukua hatua ya kuitengeneza kwa kusaini mkataba mnamo mwezi April mwaka huu (2018) na wakandarasi wa shilingi  bilioni 1.4.


Barabara za ndani za kuingia na kutoka.
Mkuu wa mkoa akiwa na mwenyeji wake mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Marry Tesha  (kushoto aliyenyoosha mkono) akikagua maendeleo ya ukarabati wa barabara ya Pamba.
Mkuu wa mkoa akiwa na mwenyeji wake mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Marry Tesha akikagua maendeleo ya ukarabati wa barabara ya Pamba.
Eneo la makutano ya kuingia kituo cha Tanganyika.
Mzee tulia, umegundua kosa lako?
Mfanyabishara huyu amepanga biashara yake ya viatu katika eneo la watembea kwa miguu barabara ya Pamba kiasi cha kusababisha watembea kwa miguu kutumia eneo la magari.
Maswali ya papo kwa hapo, maoni na ushauri. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara waliogeuza eneo la hifadhi ya barabara kuwa viota cha biashara zao. 
Bidhaa katikati ya barabara.
Muonekano wa sasa barabara ya pamba ambapo ni siku nyingi sasa ukarabati wa barabara hii, umekuwa sugu kutokana na kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara bila mafanikio yoyote, lakini tofauti na sasa katika awamu hii ya JPM ambapo makandarasi wameamua kufanya kweli.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.