ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 3, 2018

RAIS MAGUFULI AHUZUNISHWA NA MSIBA WA MAPACHA WALIUNGANA.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam January 6, 2018.

Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake.

Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo.


Maria na Consolata walikuwa watoto yatima, na walikuwa wakilelewa na kusomeshwa na Masista wa Maria Consolata wa Kanisa Katoliki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.