ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 14, 2018

PS3 Yaombwa iende mikoa yote Tanzania.

 Afisa TEHAMA kutoka OR TAMISEMI Mfaume Mnokote akiwasilisha mada ya matumizi ya dawati la dharura kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 jijini Mwanza
 Mmoja ya washiriki wa Mafunzo ya Epicor 10.2 akitoa msaada wa kiufundi wakati wa mafunzo hayo
 Bibi Shani Mangesho Ofisa Msimamizi wa fedha mwandamizi katika Mkoa wa Tabora akiwa katika mtihani wa kuwapima Wekahazina na Wahasibu wakati wa mafunzo ya Epicor 10.2 jijini Mwanza
Washiki wa Mafunzo, wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mfaume Mnokote hayupo pichani wakati wa somo la Msaada wa dharura wakati wa mafunzo ya Epicor 10.2 mkoani Mwanza (Picha zote na Atley Kuni wa OR TAMISEMI)

Atley Kuni na Glady Mkuchu- Mwanza
Washiriki wa Mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 kutoka mikoa nje (Non PS3 Region) ya mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta ya umma PS3 katika mkoa wa Mwanza, wameiomba Serikali ione namna itakavyoweza kukaa na wadau hao ili mradi uweze kuhudumia nchi nzima badala ya sasa ambapo upo katika Mikoa 13 na Halamshauri 93 pekee.

Ombi  hilo limetolewa na   Wekahazina pamoja Wahasibu kutoka Halmashauri za mikoa ya Tabora na Geita ambao wamekuwepo katika mafunzo ya siku nne ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (Epicor) Toleo 10.2, ambapo mara baada ya mafunzo hayo watendaji hao wataanza kuutumia mfumo huo ifikapo Julai mosi, 2018.

Nicholaus John ni Mwekahazina katika Halmashauri ya Wilaya Chato mkoani Geita, yeye anasema pamoja na uzuri wa mifumo lakini wanapendekeza kuwa mradi pia uweze kufikiria kutekeleza na kufika katika mikoa mingine ili kuweza kuleta uwiano sawia katika utekelezaji wa mifumo ya Umma .
Nicholaus anaongeza kuwa , matunda ya ukusanyaji mzuri wa mapato katika Halmashauri zao umetokana na kuwa na mifumo imara ambayo inasimamiwa na TAMISEMI lakini pia ufadhili kutoka kwa Shirika la Misaada la  Marekani (USAID)  kupitia mardi wa PS3.

Akitoa maoni yake Shani Mangesho, Afisa Msimamizi wa fedha katika Mkoa wa Tabora anakiri kuwa PS3 imefanya kazi kubwa kwenye mifumo lakini bado wanayohamu yakuona mradi huo unaongeza eneo la ufadhili.

Mbali yakuomba mradi huo uweze kwenda nchi nzima, lakini Wekahazina hao na Wahasibu hawakusita kuelezea furaha yao ya mabadiliko ya mara kwa mara yanayoendelea kufanywa na Serikali hasa katika kuimarisha mifumo ya Sekta ya umma.

Zablon Nashokigwa Mwekahazina Halmashauri ya  Wilaya ya urambo, alisema mafunzo ya Epicor 10.2 kwa wataalam wa kada za wahasibu yamekuja kwa wakati muafaka kwakuwa mifumo mingi sasa itafungamanishwa na mfumo huo.

“Nawashukuru TAMISEMI na PS3 katika kutujengea uwezo, hii kwetu itakuwa chachu ya uboreshaji wa shughuli zetu za kila siku hasa katika eneo la upatikanaji wa taarifa kwa muda muafaka.Kutokana na mfumo huu kuwa Kimtandao (Web based) ambao utamwezesha mtendaji kufanya kazi mahali popote ambapo yupo tofauti na mfumo ambao tunakwenda kuachana nao ifikiapo Julai Mosi,” amesema Nashokigwa.

Marietha Masanja kutoka Halmashauri ya Geita Mji amesema“Katika Epicor.10.2 hakutakuwa na hundi isipokuwa malipo yote yatafanyika kwa mfumo wa (Tanzania Interbank Settlement System-TISS) ambayo imeunganishwa kwenye mfumo huu ulioboreshwa, hivyo itawaepusha wahasibu na jukumu la kubeba pesa taslimu” alisema Marietha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.