ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 10, 2018

DKT TIZEBA AAGIZA KUKAMATWA KIONGOZI WA AMKOS ALIYEFUJA MILIONI 23

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba  akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba  akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula.
Kituo cha ukusanyaji na ununuzi wa pamba katika kijiji na Kata ya Msai, Wilayani Iramba

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula akitoa salamu za shukrani kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kufanya ziara ya kuwatembelea  wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, 

Na Mathias Canal-WK, Singida

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Mrakibu wa polisi Wilaya ya Iramba ASP Magoma Mtani kumkamata aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha ushirika (AMKOS) Msai.

Waziri Tizeba ametoa agizo hilo jana 9 June 2018 Mara baada ya kutembelea kitongoji cha Kati, Msai na Mtoa akiwa katika ziara ya kikazi ya Siku mbili kwa ajili ya kutembelea vituo vya ununuzi wa pamba na kujionea msimu wa ununuzi wa zao hilo katika vijiji hivyo.

Dkt Tizeba amelaani vikali ufujaji huo wa fedha za wakulima huku akimtaja Paul Ramadhan Kurwa kuhusika na ufujaji huo wa shilingi milioni 23 huku akiendelea kuonekana mtaani pasina kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Wakati muelekeo wa serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli ukijipambanua kutaka kuboresha maisha ya watanzania kupitia Kilimo lakini kuna watu wanataka kurudisha nyuma juhudi hizo, hakika tutawapa kibano kweli kweli hakuna utani kwenye fedha za wananchi" Alikaririwa Dkt Tizeba

Mhe Tizeba ametoa siku moja kukamatwa kwa mwizi huyo na kufikishwa mahakamani ili awe mfano kwa wezi wengine wasio kuwa na haya wala soni.

Aidha, amewataka wananchi katika msimu huu wa uuzaji na ununuzi wa Pamba kutouza Pamba zenye uchafu wakidhani wataongeza idadi ya kilo kwani kufanya hivyo ni kufifihisha juhudi zao wenyewe jambo ambalo halina tija.

Sambamba na hayo pia amewaondoa hofu wakulima kote nchini kuwa serikali ya awamu ya tano inatekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yenye mkataba na wananchi katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula amempongeza Waziri Tizeba kwa kutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea ununuzi wa Pamba huku akiwasihi wananchi wilayani humo kulima kiasi kikubwa cha Pamba msimu ujao kwani mbegu na madawa ya kuulia wadudu vitatolewa bure kuanzia msimu ujao wa mwaka 2018/2019.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.