ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 21, 2018

TIMU YA TSC YA JIJINI MWANZA YALETA TENA USHINDI NYUMBANI KOMBE LA DUNIA

NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Timu ya soka ya wasichana wanaoishi katika mazingira magumu TSC Sport Academy (Tanzania Street Children) ya Jijini Mwanza imepokelewa kwa kishindo hii leo katika uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kutwaa nafasi ya pili ya michuano ya kombe la dunia 2018 ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Urusi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella ameongoza mapokezi hayo ambapo amesema hatua hiyo inapaswa kuleta changamoto kwa timu nyingine kufanya vizuri katika michuano mbalimbali huku akiwahimiza wadau wa michezo kushirikiana na serikali kuendeleza michezo mkoani Mwanza.
 Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL na mlezi wa timu hiyo, Altaf Mansoor ameipongeza kwa ushindi huo na kubainisha kwamba TSC imekuwa kitovu cha kuibua na kuendeleza wachezaji wengi na baadhi yao wanachezea timu mbalimbali ikiwemo Simba huku wengine wakipata fursa ya za kimasomo.
 Michuano hiyo imemalizika nchini Urusi ambapo timu ya wasichana TSN imeshika nafasi ya pili baada ya kufungwa kwa tabu goli 1-0 na wenzao kutoka nchini Brazir.
Itakumbukwa mwaka 2010 nchini Afrika Kusini timu wavulana TSC ilishika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo, mwaka 2014 ikabeba kombe nchini Brazir.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.